Posts

Showing posts with the label MICHEZO

FIFA yaifungia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

Image
 S hirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi kuifungia Congo DR uanachama wake kwa muda usijulikana kutokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo na kusababisha vifo. Kwa maana hiyo Congo DR timu yao ya Taifa, Vilabu vyao na Viongozi wao hawataruhusiwa kushiriki michezo yoyote ya Kimataifa (CHAN, AFCON, CAFCL, CAFCC, Kombe la Dunia) hadi adhabu hiyo itakapoondolewa.   Reactions:

Kocha Singida BS avutwa Yanga kumrithi Ramovic

Image
Muda mfupi baada ya kocha Sead Ramovic kubwaga manyanga, Yanga leo, Februari 4, 2025 imetangaza kumchukua kocha wa Singida Black Stars, Hamdi Miloud kuziba pengo lililoachwa na Mjerumani huyo. Taarifa iliyotolewa na Yanga imesema kuwa Ramovic ameondoka sambamba na msaidizi wake Mustafa Kodro. “Uongozi wa Klabu ya Young Africans SC umefikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba na Kocha Sead Ramovic na msaidizi wake Mustafa Kodro.   “Katika hatua nyingine, Klabu ya Young Africans SC inamtangaza Kocha wake mpya, Miloud Hamdi mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa. “Kocha Hamdi mwenye uzoefu mkubwa wa kufundisha soka akiwa amefanya kazi barani Ulaya, Asia na Afrika, anaungana na timu mara moja kuanza majukumu yake mapya. “Kocha huyo mbali na uzoefu alionao, pia ana mafanikio makubwa katika soka la Afrika akishinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2015-2016 akiwa na USM Alger,” imefafanua taarifa hiyo ya Yanga. Miloud anajiunga na Yan...

Fedha Alizowekewa Mzize na Timu ya Al Ittihad hizi hapa

Image
  Klabu ya Al Ittihad ya ligi kuu soka nchini Liby imetenga ada ya uhamisho ya zaidi ya TSh bilioni 3 kwaajili kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Yanga Clement Mzize ambaye amewaka sana kwa siku za karibuni. Al Ittihad mbali na fungu hilo la uhamisho wamemuwekea mezani Mzize ada binafsi ya kusaini mkataba (sign-on fee) ni zaidi ya TSh bilioni 1.3 na mshahara wa Tsh Milioni 50 kwa mwezi huku wakimshawishi kusaini mktaba wa miaka miwili kinda huyo wa zamani wa timu za vijana za Yanga. Wakati hayo yakiendelea nje ya uwanja, Mzize ndiyo kwanza ananogesha biashara na kuwapa presha waarabu hao baada ya jana kufunga goli moja kati ya manne waliyoshinda dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara

CLEMENT MZIZE NA STEPHEN AZIZI K HAOOO AL ITTHAD

Image
  Klabu ya Al Itthad ya nchini Libya imeonesha nia ya dhati ya kupata huduma za wachezaji wawili tegemeo wa Yanga CLEMENT MZIZE NA STEPHEN AZIZI K ,kulingana na dau ambalo inasemekana wameliweka ili kupata saini za wachezaji hao ifikapo june 2025,, Kama ambavyo ananukuliwa mwandishi maarufu wa habari za michezo nchini Ghana MICKJR "Al Ittihad has reached an agreement with Yanga to transfer Clement Mzize and Stéphane Aziz to the Libyan giants. Understand; It was a 𝐜𝐫𝐚𝐳𝐲 offer that’s very difficult to turn down by the reigning champions in Tanzania. Club to club agreement is done but the move can only happen in June — the wish of Yanga. Ittihad now needs to negotiate with both players for salary structure, bonuses and working conditions. One player is keen on the move, but the other one is reluctant. More updates to come soon."

KLABU YA SIMBA YAWAOMBEA URAIA WACHEZAJI WAKE 9 TISA

Image
  Klabu ya Simba imewaombea uraia wa Tanzania wachezaji wake 9 ambao sio raia wa Tanzania. Simba SC imemuandikia Kamishina Jenerali wa Uhamiaji barua leo tarehe 23 Januari 2025, barua ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa klabu Murtaza Ally Mangungu

WACHEZAJI WATATU SINGIDA BLACK STARS WAPEWA URAIA NA UHAMIAJI

Image
  Wachezaji watatu wa Singida big stars ambao ni  EMMANUEL KWAME KEYEKEH JOSEPHAT ARTHUR BADA MUHAMED DAMARO CAMARA, Ambao waliomba nz wamepewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya sheria ya uraia ya Tanzania , sura ya 357. Kwa muktadha huo kama taarifa ilivyovyotolewa na Idara ya uhamiaji  watajwa hapo juu ni Raia wa TANZANIA KWA TAJNISI.

SHIRIKISHO LA MPIRA AFRIKA (CAF)LAIFUNGIA KLABU YA SIMBA

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeifungia klabu ya Simba Sc kuingiza mashabiki kwenye mechi yao ya mwisho ya hatua ya Makundi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Constantine Jumapili hii Januari 19, 2025. Hii ni kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mchezo dhid ya SC Sfaxien ya Tunisia uliopigwa Desemba 2024 hvyo mechi dhid ya SC Constantine itachezwa bila mashabiki katika dimba la Benjamin Mkapa. #KitengeSports

WACHAMBUZI: Wachezaji Wengi wa Ligi Kuu Wana BETI Mechi zao

Image
  Mchambuzi Edga Kibwana amepenyezewa taarifa na mdau kuwa kuna baadhi ya wachezaji wa Ligi kuu wamekuwa wakibet mechi zao hali inayopelekea Ligi kuwa na matukio mengi ya kustaajabisha. Mdau anaziomba mamlaka zinazohusika na Soka kuanza kuchunguza taarifa hizi ili kuwabaini Kutoka kwa Amri Kiemba: “Sisi tunaongea huku tunacheka lakini hali ni mbaya , inawezeka tupo hapa tunasema waamuzi waongezewe ujuzi kumbe wao nyuma wanabet” Katika kuipa uzito hoja yake Kiemba amesema unaweza kushangaa goli ni offside ya wazi lakini mwamuzi anaacha kwa sababu ameweka GG Chanzo:udakuspecial

BONDIA HASSAN MGAYA AFARIKI BAADA YA KUPIGWA "TKO"

Image
  Bondia Hassan Mgaya amefariki dunia baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi sita lililofanyika usiku wa Desemba 28, 2024 ukumbi wa Dunia ndogo Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam. Mgaya alicheza pambano hilo ambalo halikua la ubingwa na kupigwa TKO katika raundi ya sita dhidi ya aliyekua mpinzani wake Paulo Elias. Inaelezwa kuwa Mgaya alipigwa na kwenda chini kisha mwamuzi akamhesabia na baada ya mwamuzi kumaliza kuhesabu marehemu akatembea hatua kadhaa hapohapo ulingoni kisha akaanguka na kuzimia. Baada ya kuzimia marehemu akapewa huduma ya kwanza kutoka kwa madakatari waliokuwepo kwenye pambano na akazinduka kisha akapelekwa hospitali ya Sinza kwa ajili ya matibabu, Alipofikishwa hospitali ya Sinza akapatiwa rufaa ya kupelekwa hospital ya Mwananyamala na ndipo umauti ulipomkuta. Kwa upande wake, bondia Cosmas Cheka kutoka chama cha mabondia nchini, amesema kuwa wapo mbioni kuandaa utaratibu wa kumsimamisha muandaaji wa pambano hilo Haji Ngoswe kwa kutoonyesha ushirik...

Jean Baleke Apotea Kusiko Julikana, Mazoezini na Yanga Haendi Tena...

Image
  MSHAMBULIAJI wa Yanga Jean Baleke amejiweka karibu na mlango mgumu wa kutokea baada ya kukacha mazoezi ya timu hiyo. Baleke hajaonekana ndani ya kambi ya Yanga kwa zaidi ya wiki moja akikosa ratiba zote za mazoezi ya timu hiyo huku pia hata uwanjani akikosekana. . Mshambuliaji huyo alikuwa katika msafara wa Yanga ikiifuata MC Alger ya Algeria kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hakukaa hata benchini. Baada ya hapo Baleke ambaye anaichezea Yanga kwa mkopo hajaonekana tena kwenye kambi ya Yanga. CHANZO: https://www.udakuspecially.com/

Uhispania, Ureno na Morocco Wathibitishwa kuwa Wenyeji kombe la Dunia 2030

Image
  Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limethibitisha kuipatia Saudi Arabia haki za kuwa nchi mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA la 2034 huku Uhispania, Ureno na Morocco wakithibitishwa kuwa wenyeji wenza wa kombe la Dunia la mwaka 2030 Uamuzi huo umetolewa wakati wa mkutano wa FIFA leo huku mashindano hayo yakitarajiwa kufanyika wakati wa miezi miwili ya baridi ili kuepuka joto kali la kiangazi kama iliyofanyika wakati wa Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar. Aidha michuano ya Kombe la Dunia la 2030 itazishuhudia Mataifa ya Uruguay, Argentina na Paraguay zikiandaa mechi moja kila moja. Wakati uamuzi huo ukifikiwa Rais wa FIFA, Gianni Infantino alihoji: “Ni njia gani bora ya kusherehekea miaka 100 ya Kombe la Dunia kuliko hii ya kuwa na Kombe la Dunia katika nchi sita, katika mabara matatu na timu 48?” Mechi tatu za ufunguzi wa michuano hiyo ya 2030 zitapigwa nchini Uruguay, Argentina na Paraguay huku FIFA ikipanga kusherehekea miaka 100 tangu Kombe la Dunia la kwanza. Mechi zingine zi...

Yanga Waona Isiwe Tabu Waamua Kumrejesha Kocha Cedric kaze Jangwani....

Image
  Aliyewahi kuwa kocha wa klab ya YangaSc Cedric Kaze anarejea ndani ya klab hiyo. Cedric kaze anarejea kikosini humo kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Saed Ramovic, Muda wowote kuanzia sasa Kocha Kaze atawaaga wachezaji wa klab yake ya sasa ya Kaizer Chiefs na kuanza safari ya Kuja Tanzania kuanza majukumu yake mapya ndani ya waajiri wake wa zamani Young Africans.

FADLU Afunguka: Kwa Kweli, Kucheza Nyumbani ni Faida kubwa kwetu, Lazima Tushinde

Image
  “Kwa kweli, kucheza nyumbani ni faida kubwa kwetu. Tutakuwa na programu za mazoezi kwa siku chache zilizopo mbele yetu ili kuwa tayari kwa mchezo huu. Nitahakikisha mpango wetu wa kimbinu ni tofauti na ule tulioutumia kule Algeria.” “Nidhamu ya kulinda itakuwa sehemu muhimu ya mchezo wetu, lakini tunahitaji kuwa na mashambulizi ya haraka na kuzuia makosa tuliyofanya kwenye mchezo wa awali, Lengo ni kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri na kuweka hesabu zetu sawa katika michuano hii ya CAF.”

TAIFA STARS INAWEZA KUONDOLEWA KUSHIRIKI MICHUANO YA AFCON 2025,,, KWA SABABU HIZI HAPA....?

Image
  Huenda timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS ikakumbwa na adhabu ya kuondolewa katika michuano ya AFCON 2025, Kwa kosa la kumuingiza mchezaji IBRAIMU AME akiwa amevalia Jezi nambari  ''26'' lakini katika orodha iliyowasilishwa CAF hakunamchezaji mwenye jezi nambari ''26''  Kama ambavyo Guinea walivyoripoti  Shirikisho la mpira CAF. TUENDELEE KUFUATILIA  Tundumazone.blogspot.c0m

Yanga Kumsajili Mshambuliaji Huyu Kutoka Uganda...Noma na Nusu

Image
  YANGA imeanza mikakati ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba 15 mwaka huu ambapo jina la mshambuliaji Bayo Aziz Fahad ndio kipaumbele chao cha kwanza. Bayo mwenye umri wa miaka 26, inaripotiwa kuwa ameshafanya mazungmzo na kumalizana na vigogo wa Yanga ambapo wamefikia pazuri huku kilichobaki kwa mchezaji huyo ni kusubiri dirisha dogo ili ajiunge nayo. Uwezo wa kufunga na kupiga pasi za mwisho ambao Bayo amekuwa nao unaonekana kuiridhisha Yanga ambayo ujio wa mshambuliaji huyo utasaidia safu yake ya ushambuliaji lakini pia kuwaongezea ushindani chanya washambuliaji waliopo kikosini ambao wanaonekana bado wanajitafuta. Kwa sasa, Bayo ni mchezaji huru baada ya kuachana na MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Czech ambayo aliichezea mechi 42 na kuifungia mabao manane. Kabla ya kujiunga na Vyskov, Bayo aliitumikia Ashdod inayoshiriki Ligi Kuu ya Israel ambako katika mechi 41 alizoichezea, alifunga mabao manane...

HATIMAYE Yanga Wamtangaza Kocha Huyu Mpya

Image
  Yanga SC wamemtangaza rasmi  Sead Ramovic  (45) Raia wa Ujerumani kuwa Kocha wao Mkuu akija kuchukua mikoba ya Miguel Gamond ambaye amefutwa kazi na Yanga SC saa chache zilizopita. Sead anajiunga na Yanga akitokea TS Galaxy ya Afrika Kusini aliyodumu nayo kwa miaka mitatu 2021-2024 kabla ya kujiunga na Yanga SC ya Tanzania. Sead hana uzoefu sana wa soka la Afrika lakini wasifu wake unaonesha amewahi kucheza soka katika vilabu vikubwa vya Ligi Kuu Ujerumani kama VFL Wolfsburg na Borussia Mongladbach.

Mambo Matano Yanayoivuruga Klabu ya Yanga kwa Sasa.

Image
  Mambo yameendelea kuwa magumu klabu ya Yanga baada ya kukumbwa na misukosuko mingi ndani ya muda mfupi. Leo tarehe 15 Novemba Yanga wametangaza kuachana na waliokuwa makocha wa klabu hiyo ambao ni Miguel Gamondi kocha mkuu na Mousa Ndauw kocha msaidizi. Hizi ni nyakati mbaya kwa klabu hiyo na kuna uwezekano likawa anguko la klabu hiyo katika mbio za kutetea ubingwa wa ligi ya NBC na kombe la CRDB. Nimekuandalia mambo matano yanayoivuruga klabu ya Yanga kwa sasa. 1.Kufungwa na Azam pamoja na Tabora United Klabu ya Yanga ilianza vyema msimu wa 2024/25 kwa kushinda mechi 8 za awali na kuwa kinara kwenye msimamo wa ligi wakijikusanyia alama 24 na katika mechi hizo walifunga mabao 14.Mchezo dhidi ya Azam walipoteza kwa bao 1-0 na mchezo dhidi ya Tabora United walipoteza kwa mabao 3-1.Kupoteza michezo hiyo kuliibua gumzo klabuni hapo na hoja ya kumfukuza kocha Gamondi ilianza kuchochewa moto na hatimaye leo ametimuliwa. Kama umetazama michezo hii miwili ambayo Yanga wamepoteza utagundu...

WACHEZAJI AL AHLY TRIPOLI WAKATWA MISHAHARA MIEZI MIWILI KISA SIMBA

Image
Al Ahly Tripoli ya libya wameamua kuwakata mishahara ya miezi miwili wachezaji wao kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kuondoshwa kwenye kombe la Shirikisho na klabu ya Simba ya Tanzania . Kabla ya tukio hili la kukata mishahara kwa wachezaji bodi ya Al Ahly Tripoli iliwafuta kazi makocha wake wote mapema baada ya kutolewa na Simba kwenye kombe la shirikisho.

HIKI HAPA KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOMENYANA NA DRC CONGO

Image
  HICHI HAPA KIKOSI CHA WACHEZAJI WALIOITWA TAIFA STARS, SAMATTA ARUDISHWA.  Kikosi cha Timu ya Taifa @taifastars_ kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 vs DR Congo  Mechi ya kwanza itapigwa Oktoba 10, 2024, Stars ikianzia ugenini na mechi ya pili ni Oktoba 15 ambapo itapigwa Tanzania. CHANZO: UDAKUSPECIAL

Elie Mpanzu atambulishwa Simba

Image
 Karibu simba Mpanzu Elie 🦁. Simba Sports Club rasmi wamemtambulisha usajili wa Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo Elie Mpanzu Kibisawala (22)🇨🇩  kwa mkataba wa miaka miwili.