HATIMAYE Yanga Wamtangaza Kocha Huyu Mpya

 





Yanga SC wamemtangaza rasmi Sead Ramovic (45) Raia wa Ujerumani kuwa Kocha wao Mkuu akija kuchukua mikoba ya Miguel Gamond ambaye amefutwa kazi na Yanga SC saa chache zilizopita.

Sead anajiunga na Yanga akitokea TS Galaxy ya Afrika Kusini aliyodumu nayo kwa miaka mitatu 2021-2024 kabla ya kujiunga na Yanga SC ya Tanzania.

Sead hana uzoefu sana wa soka la Afrika lakini wasifu wake unaonesha amewahi kucheza soka katika vilabu vikubwa vya Ligi Kuu Ujerumani kama VFL Wolfsburg na Borussia Mongladbach.

Comments

Popular posts from this blog

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

APPLICATIONS hizi HAPA haziruhusiwi kutoa mikopo mtandaoni

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO