Posts

Showing posts with the label AFYA

Wawili wathibitika kuwa na ugonjwa wa mpox

Image
    Picha: Mtandao ugonjwa wa mpox. Wizara ya Afya imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa Mpox nchini, ambapo hadi sasa watu wawili wameugua, mmoja wao akiwa dereva wa magari ya mizigo aliyetoka nchi jirani kuelekea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Jenister Mhagama, kupitia mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa, walipokea taarifa za wagonjwa wenye vipele usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili, pamoja na homa, maumivu ya kichwa, vidonda kooni na maumivu ya misuli. Baada ya uchunguzi wa sampuli katika Maabara ya Taifa, Machi 9 mwaka huu, vipimo vilithibitisha maambukizi ya Mpox.

Hii hapa namna ya kujikinga na Mpox

Image
Picha: Mpigapicha Wetu Fahamu namna ya kujikinga na Mpox. Wizara ya Afya imewahimiza wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox kwa kuepuka kushiriki vitu vya binafsi kama nguo, mashuka na blanketi vilivyotumiwa na mtu mwenye dalili za ugonjwa huo. Pia, wananchi wanashauriwa kuepuka kugusana, kushikana mikono, kubusiana, kukumbatiana au kujamiiana na mtu mwenye dalili za Mpox. Aidha, inasisitizwa kuepuka kugusa majimaji ya mwili ya mgonjwa au kumhudumia bila kuchukua tahadhari zinazostahili. Wizara imewataka watumishi wa afya kuzingatia kanuni za kujikinga na magonjwa wanapowahudumia wagonjwa, hususan wale wenye dalili za vipele na homa. Tahadhari nyingine ni kuhakikisha unawanawa mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni au kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na maambukizi. Wagonjwa Wawili Wathibitishwa Kuwa na Mpox Katika taarifa iliyotolewa leo Machi 9, 2025, na Waziri wa Afya, Jenister Mhagama, watu wawili wamethibitika kuwa na ugonjwa wa Mpox. Mmoja wa wagonjwa hao ni de...

Miaka mitano ya Covid-19: Fahamu nchi ambazo hazikufungia watu ndani

Image
  Mnamo Machi 2020, mamilioni ya watu duniani walijikuta wamefungiwa majumbani mwao huku Covid-19 ikienea kwa kasi kubwa. Nchi kadhaa hazikuweka vizuizi, hivyo je, maamuzi yao yalikuwa sahihi? Mnamo Machi 2020, mamilioni ya watu walitumia madirisha yao kuchungulia nje. Ghafla walijikuta wamefungiwa majumbani mwao, maisha yao yabadilika kwa haraka hadi kuwa ndani ya kuta nne na skrini za kompyuta. Katika mataifa mengi, viongozi wa kitaifa walionekana kwenye televisheni wakihimiza watu kusalia makwao iipokuwa tu –wakati wa kununua bidhaa muhimu au kwa mazoezi ya kila siku. Ilikuwa ni juhudi ya mwisho ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya kutisha ambavyo tayari vilikuwa vimeua maelfu ya watu duniani kote. London, Tony Beckingham na mpenzi wake walifanya mazoezi yao ya kila siku wakiendesha baiskeli hadi katikati ya jiji jioni moja. "Tulifikiri mazingira yatakuwa yakufurahisha kuona hakuna mtu," anasema. Ilikuwa tofauti. Maeneo waliyoyajua vizuri, kama Piccadilly Circus na Le...

Prof. Janabi: Unapokunywa chai ulikuwa na njaa? Chai sio lazima

Image
  MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amesema jamii inapaswa kuwa makini na aina ya mlo, kwa kuwa hata unywaji chai asubuhi, watu wengi hunywa bila kuhisi njaa. "Chai sio lazima. ‘Breakfast’ maana yake vunja funga. Nakula matunda sita mchana. Au chai kavu, ukiweka tofauti kati ya mlo mmoja Hadi mwingine ndivyo unavyopunguza simu mwilini.  "Unachuja sumu mwilini. Mimi naagiza chai bila sukari au kunywa kahawa, naweza kuanzia mlo saa sita mchana tangu nimekula jana usiku. Amesema kwamba mara nyingi mtu anakunywa chai asubuhi kwa kufuata utaratibu uliozoeleka, ingawa  binadamu huwa haamki na njaa, iwapo alipata mlo usiku. Bingwa huyo ambaye aliyebobea katika magonjwa ya moyo, ameshauri mambo matano, ikiwamo kila mmoja kufahamu kiwango cha presha yake; kujua uzito ukoje; kujua kiwango cha sukari; na kiwango cha ukubwa wa kiuno chake. Prof. Janabi, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma zinazotolewa na ...

Majaliwa: Theluthi moja ya watoto nchini wana udumavu

Image
    Picha: Mpigapicha Wetu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi nchini na kimataifa bado kuna tatizo kubwa la udumavu ambako theruthi moja ya watoto nchini wana udumavu. Majaliwa alitoa kauli hiyo leo Alhamisi mkoani Mwanza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 10 wa Wadau wa Lishe nchini. Ameeleza kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Tanzania Demographic Health Survey (TDHS) mwaka 2018 inaonesha kuwa theruthi ya watoto nchini wamedumaa. Amesema licha ya tatizo hilo bado kuna ongezeko la magonjwa sugu yasiyoambukiza yanayotokana na lishe duni hivyo kuwataka wadau kuongeza nguvu katika utekeleza wa malengo ya afua ya lishe. Aidha, amesema kutokana na tatizo hilo upo umuhimu wa wadau mbalimbali kuandaa mjadala mpana wa kitaifa, ili kuleta msisitizo katika utekelezaji wa mipango ambayo tayari imewekwa na serikali pamoja na wadau mbalimbali. Kadhalika ameag...

Uoteshaji nywele wenye kipara wawavutia wengi Muhimbili

Image
KITENGO cha Upasuaji Rekebishi na Upasuaji wa Urembo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kinafanya upasuaji wa aina hiyo kwa wagonjwa 12 hadi 15 kwa wiki, huku mahitaji yakiendelea kuongezeka. Huduma zinazofanywa mara kwa mara ni pamoja na upasuaji rekebishi kwa majeruhi wa ajali za viwandani, barabarani, matukio ya moto; kukiwa na wastani wa wateja (wagonjwa) sita hadi wanane kwa siku. Hospitali hiyo ya hadhi ya juu zaidi kitaifa imesema kuwa miongoni mwa wanaohitaji huduma ya upasuaji rekebishi na idadi yao ni kubwa, ni wanaume wenye kipara. Bingwa wa Upasuaji Rekebishi na Upasuaji Urembo MNH, Dk. Edwin Mrema, aliyasema hayo wiki iliyopita alipozungumza na Nipashe, jijini Dar es Salaam. Mwandishi wa gazeti hili alitaka kufahamu kuhusu huduma zinazotolewa katika kitengo hicho. Alisema nchini hivi sasa ina wataalamu 10 pekee waliobobea katika upasuaji rekebishi na upasuaji wa urembo. Alisema kitengo chao kimejikita kufanya urekebishaji wa mwonekano wa mwili, hususan wa nje kwa wa...