STORY YA KIJANA HUYU AKIWA "KISIWANI" ITAKUFUZA KITU
Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake, wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao, maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana ambako hakukuwa na watu wala wanyama isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala panga, hatimaye akaanza maisha mapya. Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki. Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi. Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida. Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake ...