Posts

Showing posts with the label KITAIFA

Kiongozi Mbio za Mwenge asisitiza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Image
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ussi, ametoa wito kwa wananchi kuendeleza amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Ussi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika Wilaya ya Rufiji wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusambaza ujumbe wa kitaifa wa Mbio hizo. Aliwahimiza wananchi kuzingatia ujumbe wa mwaka huu unaosema: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu,” akisisitiza kuwa uchaguzi uwe huru, wa haki na wa kumalizika kwa amani kama ilivyopangwa na taifa. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), alisema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa chachu ya maendeleo nchini kwa kufika katika kila pembe ya Tanzania kukagua na kuchochea utekelezaji wa miradi inayogusa maisha ya wananchi. “Tu...

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

Image
  BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka Watanzania kuanza kubadili mtazamo na kuziona taka kama fursa ya kuzirejeleza na kupata bidhaa mbalimbali na kujikomboa kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa jana, jijini Dar es Salaam na Meneja Utekelezaji wa Sheria wa baraza hilo, Amina Kibola, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amezungumza wakati akizungumzia siku ya kimataifa ya Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Taka, ambayo huadhimishwa kila Machi 30 kila mwaka. Anasema hata kauli mbiu ya mwaka huu, inaweka msisitizo wa kuwa taka si uchafu bali ni malighafi yenye thamani, endapo itasimamiwa na kutumika vyema. Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Amina Kibola, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kibola amesema siku hiyo  ilianzishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 2022, ili kukuza mifumo endelevu ya matumizi na uzalishaji na kuongeza uelewa kuhusu udhibiti wa taka. Anasema siku hiyo pia ilianzishwa kwa len...

Mwalimu Mkuu akamatwa tuhuma za kubaka mwanafunzi Kilosa

Image
Mkuu  wa Shule ya Sekondari Zombo, wilayani Kilosa, Mwalimu Mkame Living Mwaisumo (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,  SACP Alex Mkama , amesema tukio hilo lilitokea  Machi 19, 2025 , ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu, ambako mwanafunzi huyo alikuwa ameagizwa kupeleka mwongozo wa somo (lesson plan). Kamanda Mkama alieleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa tukio hilo limetokana na  mmomonyoko wa maadili , huku uchunguzi wa kina ukiendelea ili kukamilisha hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa. DEREVA ALIYEIBA MAFUTA NA KULICHOMA LORI AKAMATWA Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi limemkamata  Abubakar Adam Mwichangwe (29) , mkazi wa  Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam , aliyekuwa akisakwa kwa tuhuma za  wizi wa mafuta ya Dizeli lita 35,700  na kuchoma lori alilokuwa akiendesha ili kuonekana kama ajali. Kamanda Mkama amesema kuwa mtuhumiw...

Ulega awasimamisha kazi watumishi mizani waliomnyanyasa dereva Pamela

Image
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametangaza kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wa mizani ya barabara nzima ya kuanzia Tunduma (Songwe) hadi Vigwaza (Pwani) waliokuwa zamu Machi 13 mwaka huu kufuatia kuibuka kwa mvutano kati ya watumishi wa mzani wa Vigwaza na dereva wa magari makubwa ya mizigo aliyefahamika kwa jina la Pamela. Katika picha mjongeo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionesha dereva huyo wa magari makubwa ya mizigo ambaye anafanya kazi kwenye kampuni ya Simba Logistics akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, alisimulia alitokea nchini Congo DRC akiwa amepakia mzigo wa tani 32 na Machi 13 mwaka huu  alipofika mzani wa Vigwaza gari lake lilizuiliwa kwa madai kuwa limezidi uzito. Kufuatia picha hiyo mjongeo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Ulega ametaja hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya yeye kushauriana na menejimenti pamoja na watalaamu mara baada ya Pamela aliyekuwa akiendesha gari lenye namba T137 DLQ na  trela...

Tume huru ya uchaguzi yabaini watu kujiandikisha zaidi ya mara moja

Image
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema imebaini uwepo wa changamoto kwa baadhi ya watu kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti wakati wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Dar es Salaam. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani, huku akibainisha hatua ambazo zinachukuliwa na tume hiyo baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika. Amesema baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika katika vituo, tume inachakata taarifa za watu wote walioandikishwa kupitia mfumo maalum wa alama za vidole ambao una uwezo wa kuwabaini wapiga kura wote waliojiandikisha zaidi ya mara moja. “Kingine tume hufanya zoezi la kulinganisha sura za watu wote walioko kwenda daftari lengo ni kubaini iwapo kuna waliojiandikisha zaidi ya mara moja. “Pia iwapo itabainika mtu amejiandikisha zaidi ya mara moja, jina na taarifa za mtu huyo, hufutwa na mfumo katika vituo vingine na kubakizwa katika kituo cha mwisho alichojiandikisha ...

Mwalimu, rafikiye wadaiwa kubaka mwanafunzi

Image
  . JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza, linawashikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Bukalu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na rafiki yake kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka 10. Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Wilbrod Mutafungwa alisema kuwa tukio la mwanafunzi huyo kubakwa na watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti tangu mwaka jana, liligundulika mwezi uliopita baada ya kudhoofika kiafya.   Mutafungwa, alisema inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walimbaka mwanafunzi huyo kati ya Oktoba 24, mwaka jana hadi Februari 2025 katika nyumba anayoishi rafiki wa mwalimu huyo.  Alisema mwalimu huyo inadaiwa kuwa  alimuita mwanafunzi huyo nyumbani kwake mwezi uliopita kwa kisingizio cha kumfundisha masomo ya ziada na kumbaka.  Kamanda huyo, alisema kwa mujibu wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Februari 26, mwaka huu, asubuhi alibaini kuwa mtoto huyo afya yake imedhoofika na kuamua kumpeleka hospitali.  Alisema mama huyo alidai baada ya daktari ku...

Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai

Image
  Picha: Mpigapicha Wetu Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai Wanawake wawili wanaodhaniwa kuwa washirikina wamekamatwa alfajiri hii wakiwa watupu katika madhabahu ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. Tukio hili limeleta taharuki kubwa baada ya wanawake hao kudai walitumwa kuchukua ulimi wa marehemu aliyezikwa hivi karibuni katika makaburi ya usharika. Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na wanawake hao wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi. Mwinjilisti wa Usharika wa Nkwarungo, Jeremiah Nkya, alisema walinzi walikamata wanawake hao wakiwa na mabunda ya vitu visivyoeleweka. chanz:nipashe

"Mtaa hautaki digrii, unataka ujuzi"- Faris Buruhan

Image
  Picha: Mpigapicha Wetu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan, amewataka vijana wanaopata mafunzo ya ufundi katika vyuo vya VETA kutumia vyema ujuzi wao, akisisitiza kuwa ajira mtaani zinategemea zaidi ujuzi na utendaji kazi badala ya vyeti vya elimu ya juu. Faris ametoa kauli hiyo leo, Machi 12, 2025, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Karagwe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 16 mkoani humo. Amesema elimu ya ufundi stadi ina nafasi kubwa katika maendeleo ya taifa, kwani kinachohitajika zaidi ni maarifa ya kiufundi na uwezo wa kubuni mambo yatakayowawezesha vijana kujiajiri au kuajiriwa kwenye sekta mbalimbali. "Leo, mtaa hauhitaji digrii, PhD, wala vitabu vingi, bali unahitaji watu wa kuendesha mitambo viwandani. Mpango wa nchi ni kuwekeza kwenye viwanda, na wanaoendesha mitambo siyo wenye vyeti pek...

Watanzania 36 wahukumiwa kwa kuondoka nchini kinyume cha sheria

Image
Picha: Imani Nathaniel Watanzania 36 wahukumiwa kwa kuondoka nchini kinyume cha sheria Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Watanzania 36 kulipa faini ya shilingi 30,000 kila mmoja au kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kuondoka nchini Tanzania kinyume cha sheria na kuingia Afrika Kusini bila vibali halali. Hukumu hiyo imetolewa Jumanne, Machi 11, 2025, na Hakimu Mkazi Mwandamizi Geoffrey Mhini, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani. Katika kesi hiyo namba 72/2024, Wakili wa Serikali, Raphael Mpuya, akisoma shtaka mbele ya Hakimu Mhini, alieleza kuwa watuhumiwa 36, akiwemo Said Omary Buba (25) mkazi wa Kizuiani, Dar es Salaam, Allen Ernest William (21) mkazi wa Mwanza, Hamad Said Magimaba (25), na wenzao 33, walitumia usafiri wa barabara kupita katika mipaka isiyojulikana hadi Afrika Kusini. Wakili Mpuya alieleza kuwa watuhumiwa hao waliingia Afrika Kusini bila kufuata taratibu rasmi za uhamiaji, bila hati za kusafiria (passport), na bila kup...