Posts

Showing posts with the label SIASA

CHADEMA hatarini kufutiwa usajili

Image
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kipo katika hatari ya kufutiwa usajili iwapo kitaendelea na kuwatambua viongozi waliovuliwa uongozi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Katika barua ya Msajili iliyotoa taarifa kwa ofisi hiyo imeeleza kuwa inayo mamlaka ya kukifutia usajili chama hicho endapo kitaendelea kuwatambua viongozi hao. “Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inapenda kuwakumbusha wanachama na viongozi wa CHADEMA kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria ya Vyama vya Siasa Msajili anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa chama hicho” imesema sehemu ya barua ya Msajili. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imeendelea na msisitizo wake wa kutoitambua Sekretarieti ya uongozi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayomjumuisha Katibu Mkuu wake John Mnyika. Sekretarieti hiyo ya CHADEMA iliteuliwa Januari 22 mwaka huu kwenye Baraza Kuu la chama hicho baada ya kupatikana kwa uongozi mpya unaoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa, Tundu Lissu. cha...

Watia nia CHADEMA 55, waibuka na hoja tisa kuhusu ‘no reforms no election’

Image
Picha: Mtandao Ofisi ya CHADEMA. Watia nia 55 wa ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mwaka 2025, wakiwakilisha zaidi ya 200 walioonesha nia, akiwemo baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho, wameibuka na hoja tisa kuhusu msimamo wa chama huo wa kutoshiriki uchaguzi endapo hakutakuwa na mageuzi ya kisiasa ('No reforms, no election'). Kupitia waraka walioutuma Aprili 4, 2025 kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, watia nia hao wameeleza kuwa msimamo huo kwa sasa unakinzana na malengo yake ya awali. Wamedai kuwa haiwezekani kuzuia uchaguzi kwa kuwa nje ya mchakato huo, wakisema hatua hiyo inaweza kuchukuliwa kama kitendo cha jinai. Kwa mujibu wa waraka huo, njia pekee ya kuzuia uchaguzi isiyo huru ni kushiriki mchakato huo kwa kuingiza wagombea, ambao wanaweza kuhamasisha na kuongoza wananchi kuzuia uchaguzi katika maeneo mahsusi yenye viashiria vya hujuma, badala ya kuwa nje ya mchakato mzima. Hoja tisa kuu zilizowasilishwa: 1. ✍🏿 Mbinu ya Kuzuia Uchaguzi Kutoka ...

CHADEMA kuwapokea tena waandamizi waliowahi kukimbia chama

Image
  PICHA: MTANDAO CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), kimesema katika ziara hiyo ambayo itaanzia Kanda ya Nyasa kwa kuanzia mkoa wa Mbeya, kinatarajia kupokea wanachama wapya na miongoni mwao ni waliokuwa wanachama waandamizi wa chama hicho. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Amani Golugwa wakati akizungumza na waaandishi wa habari kutangaza kuanza ziara hizo ambayo alisema inatarajiwa kuchukua siku 47 mpaka mwanzoni mwa Mei mwaka huu.

ALAT yawataka madiwani kufanya mikutano ya hadhara

Image
Picha Maulid Mmbaga. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Murshid Nzege, (kushoto) akizungumza na waandishi leo kulia ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Murshid Nzege, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa madiwani nchini kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wananchi kuhusu maendeleo yaliyofanikishwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya mikutano ya hadhara kuanzia vitongojini, vijijini, na mitaani. Akizungumza leo jijini  Dar es Salaam , Nzege amebainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu Rais Samia aingie madarakani, yakiwemo ujenzi wa madarasa, ajira kwa madaktari na walimu, pamoja na ufanikishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Alisema ni jukumu la madiwani kuwahabarisha wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo. "Hili litawasaidia wananchi kutambua jinsi Ilani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) inavyotekelezwa kwa vitendo, kwani yapo maendeleo yanayoonekana na ...

Kada CHADEMA atangaza kugombea urais

Image
  Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Romanus Mapunda. Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Romanus Mapunda, ametangaza azma yake ya kugombea urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025. Mapunda, ambaye ni mkazi wa  Kawe, Dar es Salaam , alitoa tamko hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya  Heritage Cottage , iliyopo katika  Manispaa ya Songea . Akiwa na ari kubwa, Mapunda alisema hana sababu yoyote ya kutogombea nafasi hiyo na kwamba amejipanga kikamilifu kushiriki mchakato wa kuwania urais kupitia CHADEMA, akisubiri taratibu rasmi za chama. "Nimeamua kutangaza wazi kuwa nitachukua fomu ya kugombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA. Naomba ushirikiano kutoka kwa chama changu kwa sababu nina mpango wa kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo nchini. Nataka kuijenga Tanzania mpya yenye mwelekeo mzuri kwa wananchi,"  alisema Mapunda. Ahoji kauli mbiu ya "No Reform, No E...

Lissu, Viongozi ACT Wazalendo wazuiwa kuingia Angola

Image
  MWENYEKITI WA Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Tundu LIssu na Viongozi wa ACT Wazalendo ukiongozwa na Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Mwenyekiti wa Chama hicho, Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar umezuiwa kuingia nchini Angola na mamlaka za Serikali ya Angola. Viongozi hao kutoka Tanzania pamoja wengine kutoka nchi mbalimbali wamezuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Luanda na hati zao za kusafiria nazo zinadaiwa  kushikiliwa pia. Serikali ya Angola, bila kueleza sababu yoyote imetoa amri ya viongozi hao kurejeshwa Tanzania. Viongozi hao wa siasa kutoka Tanzania waliwasili Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (The Platform for African Democrats (PAD)] yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation yaliyopangwa kufanyika kuanzia Machi 13-16 mwaka huu. Mbali na Lissu na viongozi wa ACT Wazalendo, viongozi wengine zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali Afrika ambao pia walikuwa wanahudhuria mkutano huo wame...

Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi

Image
  Picha: Mpigapicha Wetu Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi OFISA Utumishi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Nicodemus Tindwa, amesema mchakato wa kuligawa Jiji hilo kuwa majimbo mawili ya uchaguzi umekamilika, baada ya wataalamu wa halmashauri kufanya tathmini na kubaini kuwa linakidhi vigezo vinavyotakiwa. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Tindwa, amesema Jiji la Mbeya lina tarafa mbili, kata 36, mitaa 181, na lina ukubwa wa kilomita za mraba 258.8.  Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, linakadiriwa kuwa na wakazi 141,603. Kutokana na hali hiyo, Jiji la Mbeya litakuwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Mbeya Mjini na Jimbo la Uyole.

CHADEMA kutinga mahakamani kushtaki INEC

Image
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema chama hicho kwa kushirikiana na wadau wengine, kiko kwenye mchakato wa kwenda mahakamani kuishtaki Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC). Lissu, mtaalam wa sheria na mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, amesema lengo lao ni kuzuia mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ukiwamo ugawaji majimbo uliotangazwa hivi karibuni na INEC. Alibainisha hayo jana wakati wa mahojiano maalumu na waandishi wa habari wa gazeti la Nipashe na Nipashe Digital, nyumbani kwake Tegeta mkoani Dar es Salaam. Lissu alisema tayari mchakato huo uko tayari na wakati wowote watakwenda mahakamani. "Kwanza kwenye hiyo ya tume kuanza mchakato wa kutengeneza majimbo upya, tunafungua kesi Mahakama Kuu kwa kushirikiana na wadau wengine kama Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), na mimi nimesaidia kudrafti hiyo kesi, kuomba itamke kwamba huo mchakato ni haramu, iupige marufuku. "Ni haramu kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, utarati...

Mtihani wa Lissu Chadema ni sawa na Ruto Kenya

Image
  Uchaguzi unapoisha, macho yote humtazama aliyeshinda. Matarajio huwa mengi endapo mshindi anakuwa mpya kwenye kiti. Mategemeo huwa na nguvu zaidi pale mshindi mpya anapofanikiwa kupitia agenda ya kumsiliba mtangulizi wake. Ilitokea Kenya kama mfano dhahiri. Rais William Ruto, hadi sasa bado anateswa na urais wake. Tangu alipokula kiapo kuiongoza nchi hiyo, Septemba 13, 2022, amekuwa akikumbwa na misukosuko mingi. Kuanzia maandamano ya Raila Odinga hadi ya Kizazi Z (Gen Z). <<<<<<<<<bofya hapa kusoma zaidi>>>>>>>> chanzo:mwananchi

MBOWE AKUBALI KUSHINDWA UCHAGUZI AMPONGEZA TUNDU LISSU (UENYEKITI CHADEMA)

Image
  Kupitia ukurasa wake wa twitter (x), aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA freeman mbowe, ameandika maneno yenye tafsiri ya kushindwa uchaguzi na kukubali kushindwa kwa kumpongeza mgombea mwenzake TUNDU ANTIPAS LISSU.

HISTORIA YA KIUONGOZI YA STEVEN WASIRA (MAKAMU MWENYEKITI CCM)

Image
 Steven Wasira ni mwanasiasa mashuhuri nchini Tanzania aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Mwibara akiwa na umri wa miaka 25 Historia ya Kisiasa 1. Uanachama wa TANU na CCM: Steven Wasira alianza harakati zake za kisiasa kupitia chama cha TANU kabla ya kuungana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya vyama hivyo kuunganishwa mwaka 1977. 2. Ubunge: Wasira alikuwa mbunge wa muda mrefu, akiwakilisha majimbo mbalimbali, ikiwemo Bunda na Ukerewe. Uwezo wake wa kushawishi na kujenga hoja ulimfanya kuwa mmoja wa wanasiasa maarufu ndani ya chama. 3. Wadhifa wa Uwaziri: Alishika nafasi mbalimbali za uwaziri katika serikali, ikiwemo: Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Waziri wa Mipango, Uchumi, na Uwezeshaji. Katika nafasi hizi, alihusika katika sera za maendeleo ya kilimo, uchumi, na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. 4. Mshauri na Kiongozi wa CCM: Alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CC...

Uchaguzi BAZECHA: Suzan Lymo Mwenyekiti Mpya, Hellen Kayanza Katibu Mkuu

Image
    Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA), Suzan Lymo. WAJUMBE wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA), wamepiga kura na kumchagua Suzan Lymo kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo akiwashinda washindani wengine wanne kwenye kinyang’anyiro hicho. Suzan anakuwa mwenyekiti mteule wa baraza hilo, akijikusanyia kura 96, huku miongoni mwa aliowabwaga akiwa ni mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hashim Issa, aliyepata kura 14 akitetea nafasi hiyo. Pia wamemchagua Hellen Kayanza kuwa Katibu Mkuu wa baraza hilo (BAZECHA) kwa kura 115 akiwabwaga washindani wengine wawili. Kabla ya matokeo hayo yaliyotangazwa mapema leo Jumanne Januari 14, 2025, Hellen alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa BAZECHA kwa upande wa Tanzania Bara. chanzo:globalpublishers

HAWA HAPA WAZEE 8 WATAKAOSIMAMIA UCHAGUZI CHADEMA KITAIFA(MBOWE VS TUNDU LISSU)

Image
  Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika ametangaza kamati ya wazee wanane wastaafu ambao ni wanachama wa chama hicho, wenye jukumu la kusimamia mikutano ya kitaifa ya uchaguzi wa 2025. Taarifa hiyo imeandikwa na John Mnyika kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X , ikiwataja wazee hao kuwa ni  Ahmed Rashid Alfred Kinyondo Profesa Azaveli Rwaitama Wakili Edson Mbogoro Francis Mushi Lumuli Kasyupa Profesa Raymond Mosha Ruth Mollel. Taarifa hiyo imesema uteuzi wa wazee hao umefanywa na kamati kuu katika kikao cha January 11,2025 kwa kuzingatia kanuni za chama kifungu cha 7.3.1. Chanzo: upendo media

Chadema yaonya minyukano ya wagombea

Image
Muktasari: Katibu mkuu John Mnyika aonya wanachama, wagombea na mawakala wao watakaovunja sheria na miongozo ya chama kuwa moja ya dhabu ni kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi. Dar es Salaam.  Wakati minyukano ya wazi na ya chini kwa chini ikiendelea kuelekea uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ngazi ya taifa, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika ametoa onyo kwa wanachama, wagombea na mawakala wao, akiwataka kufuata miongozo ya kampeni la sivyo hatua zitachukuliwa dhidi yao. Miongozo hiyo ni ile iliyotungwa na kuanza kutumika mwaka 2012, kuhusu taratibu za kuendesha kampeni na kujitojihusisha na vitendo vya rushwa. Amesema kwa yeyote atakayeona kuna mwanachama au mgombea anayekiuka miongozo hiyo, awasilishe malalamiko rasmi kwenye ofisi yake au kwa mamlaka zinazohusika kulingana na anayetuhumiwa, ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa haraka. Pamoja na suala hilo, Mnyika amewatangazia wagombea, wapambe na wanachama wa chama hicho, kuwa uchaguzi huo utak...