Posts

Showing posts with the label KIMATAIFA

Trump na Magufuli ni viongozi wa "damu moja" kwa aina yao ya uongozi?

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images  Imetimia miaka minne tangu John Pombe Magufuli, rais wa tano wa Tanzania afariki dunia. Alikuwa mmoja ya viongozi wachache wa Afrika waliovuma sana wakati wa uhai na uongozi wake. Alizungumzwa kila kona kwa namna alivyokuwa akiongoza nchi na watu wake wa Tanzania. Wapo waliomkosoa na wapo waliomuunga mkono kwa namna alivyozungumza, alivyotoa maamuzi na na maagizo, na jinsi alivyochukua hatua kwa masuala mbalimbali, kwananamna fulani ya ufanano kama ilivyo sasa kwa Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye wapo wanaomkoa na wapo wanaomuunga mkono kwa anayoyazungumza na kuyatenda. Baadhi ya watu wanawafananisha kwa kiasi kwa namna wanavyotawala na kuongoza mataifa yao, licha ya tofauti kubwa iliyopo kati ya Tanzania na Marekani kwenye eneo la uchumi, siasa, huduma za kijamii na hata idadi ya watu. Marekani ikiiacha mbali Tanzania kwenye kila eneo. Ingawa viongozi hao waliongoza mataifa yenye historia, tamaduni, uchumi, na siasa tofauti, wote wanasha...

Raila na Ruto wakubaliana kufanya kazi pamoja

Image
  Rais William Ruto wa Kenya na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga wameweka rasmi saini kwenye mkataba wa kisiasa, ishara ya azma yao ya kufanya kazi pamoja ndani ya serikali moja. Makubaliano hayo kati ya chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) kinachoongozwa na Ruto na chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kinachoongozwa na Raila yameelezwa kuwa yanayolenga kufanikisha malengo ya serikali. Makumi ya maelfu wa Wafuasi wa vyama vya UDA na ODM walifurika ndani na nje ya jumba la mikutano la KICC Ijumaa, jijini Nairobi wakinuia kumega kipande cha historia ambayo ilikuwa inaandikishwa kwenye madaftari ya demokrasia ya taifa la Kenya. Tukio ambalo kwa wachanganuzi wa siasa litakuwa na athari kubwa kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2027, likijiri  miezi michache baada ya Vyama hivyo kuanzisha serikali pana ya muungano. Wakisaini mktaba huo Rais ambaye anaongoza chama tawala cha UDA na Raila Odinga anayekiongoza chama cha ODM, walisema kuwa mkataba huo unalenga kukabili...

DRC yaingia mtegoni, M23 yaanzisha mashambulizi mapya yatwaa mji wa madini

Image
Siku moja baada M23 kudhaniwa kuanza kutekeleza sitisho la vita kufuatilia taarifa ya awali, suala hilo limeoneka kuwa ni mtego dhidi ya Majeshi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hii ni baada ya M23 kufanya shambulizi la kushtukiza na kuchukua Mji wa madini katika jimbo la Kivu Kusini, wakati wakiendelea kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Bukavu. Baada ya M23 inayotajwa kusaidiwa na Majeshi ya Rwanda kuuchukua mji wa kimkakati wa Goma  huko  Kivu Kaskazini, walitangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kuanza siku ya Jumanne.  Hata hivyo sitisho hilo limeoneka kuwa mtego kwa DRC kutokana na mapigano makali yaliyoanza Februari 5, 2025 na kundi hilo likitajwa kuwa na washirika wake Wanyarwanda hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.  M23 na majeshi ya Rwanda wameuchukua  mji wenye madini wa Nyabibwe, kilometa 100 kutoka  Bukavu na kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege wa jimbo hilo. Kuanzishwa kwa mashambulizi hayo mapya mash...

Kagame: Rwanda itafanya lolote kujilinda, M23 wadaiwa kusitisha mapigano

Image
  Wakati Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiapa kuurejesha Mji wa Goma, jiji lenye takriban watu milioni 3, kutoka mikononi mwa waasi wa M23, imeendelea kuishutumu Rwanda kwa madai ya kutuma wanajeshi huko kuwaunga mkono waasi hao. Hata hivyo, katika mahojiano maalumu na CNN, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye amekanusha mara kadhaa tuhuma hizo, alisema hajui kama wanajeshi wa nchi yake wako mashariki mwa Kongo ambako mapigano kati ya kundi la M23 na vikosi vya Kongo yanaendelea. Kagame alisisitiza kuwa Rwanda itafanya kila linalowezekana kujilinda, huku akiishutumu Afrika Kusini kwa madai ya kutuma wanajeshi wake mashariki mwa DRC kwa lengo la kutafuta madini. Katika hatua nyingine, Muungano wa waasi wa Alliance Fleuve Congo (AFC), unaojumuisha waasi wa M23, umetangaza kusitisha mapigano kuanzia leo Februari 4. Taarifa inayodaiwa kuwa ya kundi hilo, iliyosambaa kwenye mtandao wa X (Twitter), ilieleza kuwa usitishaji huo wa mapigano umefanyika kwa sababu za kibi...

HILI HAPA CHIMBUKO LA M 23

Image
  Chanzo cha picha, AFP Maelezo kuhusu taarifa Author, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kumeshuhudiwa mzozo na ukosefu wa utulivu …Kwa muda usiokuwa chini ya miongo mitatu. Ila katika muongo mmoja uliopita, mapigano makali yamezuka mara kwa mara. Japo eneo hilo linalojumuisha majimbo ya Ituri, Kivu kusini na Kivu Kaskazini yana jumla ya makundi ya wapiganaji zaidi ya 129, kundi la waasi la M23, ambalo ndilo kuu lililobuniwa baada ya makubaliano ya Machi 23 ya kutafuta amani imekuwa na historia ya machafuko. Pamoja na sababu za kihistoria, mashindano ya kikanda, na machafuko ya ndani, hali hiyo kwa mara nyingine tena inavuta hisia za kikanda na za kimataifa. Chanzo cha picha, AFP Kundi la M23 ni nini na lilianza vipi? Huwezi kuzungumzia M23 bila kuangazia historia ya jamii ya Watutsi katika eneo la mashairiki mwa Kongo, na ambao pia wako nchini Rwanda. Makundi mbalimbali yalibuniwa ili kutetea maslahi ya jamii ya watutsi katika eneo hilo. Mwaka 2006 CNDP (National...