Posts

Showing posts with the label ELIMU

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO

Image
  Geofrey Kiliba, mwanafunzi wa Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwa mwaka wa uongozi 2025/2026, katika uchaguzi mkuu uliofanyika leo visiwani Zanzibar. Kiliba alipata ushindi huo mkubwa kwa kuungwa mkono na kura nyingi kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAHLISO, ambao wanawakilisha serikali za wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini. Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Kiliba aliwashukuru wajumbe kwa imani waliyoionesha kwake, na kuahidi kuwa kiongozi mwenye maadili, uwazi, ushirikiano na weledi katika kutekeleza majukumu yake. Aliahidi kujenga TAHLISO imara, yenye kusikiliza na kutetea maslahi ya wanafunzi kwa nguvu na hekima. “Nitakuwa kiongozi mwenye masikio makubwa na mdomo mdogo; niko tayari kusikiliza hoja na haja zenu. Sote tuna ndoto za kuwa viongozi, lakini leo naomba mtangulize maono ili nitimize ya kwetu sote,” alisema Kiliba kwa u...

Haya hapa majina ya walimu wapya walioajiriwa serikalini

Image
  Serikali imewaita kazini walimu wapya 319 wa fani mbalimbali, ambapo halmashauri saba zimenufaika na kuongezewa nguvu kazi hiyo mpya katika sekta ya elimu. Taarifa ya kuitwa kazini kwa  walimu  hao ilitolewa jana,  Machi 12, 2025 , na  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma . Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji wa nafasi za ualimu waliofanya usaili kati ya  Septemba 4, 2024 , na  Februari 24, 2025 , wamepangiwa  vituo vya kazi  kulingana na matokeo yao. "Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuwa matokeo ya waliofaulu yanaweza kupatikana kwenye tangazo hili. Orodha hiyo pia inajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwepo kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali, ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana,"  inaeleza sehemu ya taarifa hiyo. Walimu hao wamepangiwa kufanya kazi katika halmashauri zifuatazo: ✅  Halmashauri ya ...

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.

Image
  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 29, 2024 huku matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi yakifutwa. Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Januari 23, 2025 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed jijini Dar es Salaam. Amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,” amesema Dk. Mohammed. >>>>>>>>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE<<<<<<<<

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024

Image
  Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kujipima ya darasa la nne na kidato cha pili ambapo matokeo ya jumla yanaonesha kuongezeka kwa ufaulu kwa mitihani hiyo. >>>>>>>>>>>>>>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024<<<<<<<<<<<<<

TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kujipima ya darasa la nne na kidato cha pili ambapo matokeo ya jumla yanaonesha kuongezeka kwa ufaulu kwa mitihani hiyo. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limesema jumla ya wanafunzi 1,320,227 kati ya wanafunzi 1,530,911 waliofanya mtihani wa Darasa la Nne, sawa na asilimia 86.24 wamefaulu kwa kupata madaraja A, B, C na D ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.9. NECTA imesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 699,901 sawa na asilimia 53, na wavulana ni 620,326 sawa na asilimia 47. >>>>>>>>>>>>BOFYA HAPA KUTAZAMAMATOKEO YA DARASA LA NNE<<<<<<<<<<<

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

Image
  Jumla ya  wanafunzi 974,332  waliohitimu  Elimu ya Msingi mwaka 2024  tayari wamechaguliwa na wamepangiwa  Shule za Sekondari  na wanatarajiwa kuanza masomo yao  Januari 2025 . Hii ni hatua muhimu inayolenga kuhakikisha kila mwanafunzi anapata fursa ya kuendelea na elimu ya sekondari, hatua inayochangia katika kuinua viwango vya elimu nchini . >>>>>>>>>>>>>>>>> BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA NA SHULE WALIZOPANGIWA KIDATO CHA KWANZA <<<<<<<<<<<<<<<<

TAARIFA YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WALIOKATA RUFAA

Image
  WANAFUNZI 4,676 WAPANGIWA MIKOPO YA TZS 15.5 BILIONI KWA RUFAA Upangaji wa mikopo kwa mwaka 2024/2025 wafikia mwisho Wanafunzi  4,676  wamepangiwa mikopo yenye thamani ya  TZS 15.5 bilioni  baada ya rufaa zao kufanikiwa katika mwaka wa masomo  2024/2025. Taarifa iliyotolewa leo (Jumanne, Disemba 03, 2024) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia imesema kuwa wanafunzi  4,183  ni wa mwaka wa kwanza ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya  TZS 13.8 bilioni  na wanafunzi wengine  493  ni wa mwaka wa pili na kuendelea ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya  TZS 1.7 bilioni  kwa njia ya rufaa . Aidha, taarifa hiyo ya Dkt. Kiwia inajumuisha wanafunzi  3,934  wa mwaka wa pili na kuendelea ambao wamepangiwa mikopo kwa mara ya kwanza yenye thamani ya  TZS 12.4 bilioni. “Jumla ya wanafunzi  86,646  wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya  TZS 273.46 bilioni ; kati yao ...

Picha za ngono, uhusiano vyatawala kwenye simu za wanafunzi

Image
  Picha: Mtandao Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Tabora, Nestory Mashiku. TAKRIBANI simu 120 zimekamatwa shuleni, huku zilizo nyingi zikiwa na maudhui yanayohusu ngono na uhusiano kimapenzi. Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Tabora, Nestory Mashiku, ameyasema hayo mkoani humo, na kwamba wamebaini hilo baada ya wanafunzi kukutwa na simu janja shuleni. “Tunaziona simu kama nyenzo ya kufundishia ila ni kama inaharibu watoto wetu. Mtoto ana utaalamu wa kutumia simu kuliko mzazi wake. Nilikuwa katika kikao shuleni fulani nimeshuhudia simu zaidi ya 120 zilikusnaywa, wana makundi na wanasambaza taarifa. Baadhi simu zina picha za ngono na wana-share (wanasambaza), wametengeneza na kundi, ila wengine katika simu zao wana uhusiano, wanapeana taarifa tukutane saa ngapi? Hali sio salama, kila mmoja afanye kazi yake, ulinzi na usalama wa mtoto ni wajibu wetu,” amesema Mashiku. chanzo:nipashe

Rais Samia: Sitaki ujauzito shuleni

Image
Rais Samia: Sitaki ujauzito shuleni RAIS Samia Suluhu Hassan ameonya kwamba hataki kusikia kesi za wanafunzi wameshindwa kumaliza masomo yao kutokana na ujauzito na endapo ikitokea atawakaba walimu wao. Alitoa angalizo hilo jana wakati akizindua Shule ya Sekondari Samia Suluhu Hassan iliyojengwa kata ya Rwinga, kijiji cha Migerege, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma. Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 1,000 wa kidato cha kwanza hadi cha sita. Hadi sasa wanaoendelea na masomo shuleni huko kwa kidato cha kwanza na sita ni 548. "Nisisikie kesi kwamba wanafunzi hawa wameshindwa kumaliza masomo yao kwa sababu ya ujauzito na ikitokea nitakabana shingo na walimu kwa sababu huku msituni hakuna kwa kutokea. "Walimu tunajua kazi tuliyowapeni. Changamoto zenu sisi kama serikali tunazifanyia kazi, tuko pamoja nanyi wala hatutawaacha," aliwaahidi. Rais Samia aliwataka walimu kuhakikisha wanawatunza wanafunzi hao, huku akiwaeleza kwamba Mungu amewachagua kuwa nao. ...

ORODHA YA KWANZA YA WANUFAIKA BODI YA MIKOPO 2024/2025 YATANGAZWA

Image
  Ni awamu ya kwanza yenye wanafunzi 21,509 Mikopo yao ina thamani ya TZS 70.78 bilioni Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumamosi (Septemba 28, 2024) imeanza kutangaza orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo  2024/2025.  Awamu hii ya kwanza inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ya Shahada ya awali, Shule ya Sheria kwa Vitendo na Shahada ya Uzamili. Wanafunzi kupata taarifa kupitia SIPA Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema wanafunzi wote walioomba mikopo kwa mwaka  2024/2025  wanaweza kupata taarifa za kina kuhusu mikopo yao kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama  ‘SIPA’ -  Student’s Individual Permanent Account. “Leo tumeanza kutoa taarifa za mikopo kwa makundi yote, waliopangiwa mikopo, wapo ambao bado tunaendelea kufanyia kazi maombi yao … kila mwombaji anapata taarifa yake kwenye akaunti ile ile aliyotumia kuombea mkopo, huhitaji ku...