Posts

Showing posts with the label MAHUSIANO

Apps 10 Maarufu Za Kutafuta Wachumba 2024

Image
  Tunatumia mtandao kila siku. Wengi wetu huchukua muda wao mwingi sana kuingia online na kuchat na marafiki, kupata habari, kudownload, kusoma udaku, kuangalia video nk. Kando na kutumia simu yako kuangalia video na kusoma makala tofauti tofauti, unaweza pia kutumia simu yako kutafuta wachumba. Kazi hii imerahisishwa sana kwa sababu kuna mitandao/app ambazo ni spesheli za kukunganisha na wengine. Hii hapa ni baadhi ya mitandao bora zaidi ambayo ina umaarufu zaidi barani Afrika. Mitandao ya kutafuta wachumba 1. Nipenzi Huu ni mtandao ambao una umaarufu sana nchini Tanzania na hata Kenya. Kinachotofautisha mtandao huu na mingine ni kuwa usajili na utumizi wake ni bure. Pia unaweza ukapata features nyingine kali kali ndani ya app. Kando na kuwa unaweza kuchagua lugha ya Kiswahili, utapata nafasi ya kuchat na watu tofauti tofauti  2. Zoosk Huu ni mtandao ambao wenyewe wanaupigia upato kuwa mtandao wa kutafuta wachumba unaoongoza kwa umaarufu bara la Afrika. Mtandao huu unaruhusu ...

Zijue Hatua Za Kumfanya Mwanamke Akutamani

Image
  Ungehisi vipi kama kila unapoamka asubuhi mwanamke unayemjua anakuwa wa kwanza kukutumia jumbe za kimahaba na kukuambia, "Jana sikulala, nilikuwa nakufikiria wewe"? Ama je, kila ukikutana na huyu mwanamke anakwambia, "bebi usiende, nataka muda mwingi na wewe. Nakumiss sana"? Ni raha iliyoje hii? Sasa fikiria ungekuwa na uwezo wa kufanyia hivi mwanamke yeyote yule unayekumbana naye! Ni nishati ya ajabu! Uzuri hapa Nesi Mapenzi hatukosi kuja na ujanja mpya. Fuata mbinu hizi hakika 3 ambazo zitamfanya mwanamke yeyote akutamani. #1 Kuwa wingu lisilofahamika. Hii inamaana ya kuwa usikuwe na yeye wakati wote. Kama mmepanga kukutana na yeye ili muongee kwa saa limoja, hakikisha umekaa na yeye muda wa nusu saa halafu utoe kisababu cha kujiondoa katikati ya maongezi yenu. Hii itamfanya kuachwa kwenye mataa na kutaka kujiuliza maswali kama mungekuwa naye saa zima mngeongea nini. Hii itamfanya yeye kukufikiria kwa urahisi. Lile ambalo mmeliacha kati kati litakuwa likimzunguk...

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Image
  Je wewe ni miongoni mwa wale ambao wameshawahi kupendwa na mwanamke halafu baadae mwanamke huyo akapoteza interest na wewe? Ama ushawahi kumfukuzia mwanamke halafu ukaona kuwa unafaulu lakini baada ya masiku kadhaa mwanamke huyo akapoteza interest na wewe ghafla. Hali hii hutokea wakati ambapo mwanamke huyu anaona tabia ambazo uko nazo sahizi ni tofauti na zile ambazo ulikuwa nazo awali, ama hakutarajia kukuona venye umebadilika. Somo la leo tutakufundisha jinsi ya kurudisha interest ya huyu mwanamke na aanze kukupenda kwa mara nyingine. Zama nasi! #1 Tafuta chanzo kilichosababisha mambo kuharibika. Jambo la kufanya kwanza ni kutambua mambo ambayo yalifanya hadi mwanamke huyu kuchoka na wewe. Inaweza kuwa labda mapenzi yako kwake yalikuwa yakupindukia akashindwa ama labda hakupendezwa na mwenendo ama approach yako kwake. #2 Mpe nafasi. Ameamua kukutenga. Hii ni kwa sababu amekuona huna manufaa kwake. So wewe pia lazima uheshimu maamuzi yake. So mpe nafasi yake akae kivyake. Hata ...

Jinsi Ya Kuwaepuka Wanaume Wanaokutongoza Ilhali Unawachukia

Image
Ishawahi kutokea kwa kila mwanamke ya kuwa kuna mwanaume mmoja ambaye anakutongoza ilhali unamchukia. Halafu mbaya zaidi ni kuwa mwanaume kama huyu haskii kabisa, kila ukijaribu kumkataa ndivyo anavyozidi kukuapproach. Mara nyingi huwa inaanza hivi. Anakuapproach, anakutongoza halafu unamkubali kiasi cha kuwa unataka kumsoma akili yake. Baada ya kutoka out ama deti mara kadha ukakuja kugundua kuwa mwanaume kama huyu ana matatizo flani ambayo wewe binafsi hukuyapenda. Unajaribu kumkaa mbali lakini unamwona hataki. Unajaribu kila mbinu za kumtenga lakini yeye anasistiza. Well. Wakati ni sasa wa kumwambia akuache kabisa kwa kutumia mbinu zifuatazo. #1 Mwambie kwa upole kuwa hujiskii na yeye.  Kama umegundua kuwa huyu mwanaume anayekuvizia ana matatizo lakini si tishio kwako, basi kumwambia ukweli ndio muhimu. Mwambie kuwa yeye ni mwanaume mzuri *hata kama sivyo*, lakini huko interested na yeye ndani ya moyo wako. Akiuliza ni kwanini, mwonyeshe utofauti wenu. Unaweza kumwambia kuwa wew...

SMS ZITAKAZO MNYEGEZA MWANAMKE

Image
  Kitambo nilikuwa nikipitia sms za mapenzi na kuzisoma lakini sikuona umuhimu wake. Kile kitu ambacho nilikuwa nikiaminia ni mistari yangu ambayo nitaimwaga mbele ya mwanamke. Katika maswala ya kutumia sms za mahaba hazikunigonga kichwa kabisa. So siku moja katika pitapita zangu katika mitandao, nikakumbana na meseji moja nzuri nikaona hebu nijaribu uwezo wa meseji hii. Meseji yenyewe ilikuwa inasema hivi, "Itunze meseji hii kwa kuwa ni uthibitisho wa penzi langu kwako". Kimzaha nikamtumia mpenzi wangu aliyekuwa yuko mbali na mimi. Akajibu kupitia sms, "Asante mpenzi wangu. Nashukuru kwa mapenzi yako". Kwa kuwa sikutilia maanani na nilikuwa naamini meseji za mahaba hazina umuhimu wowote, sikushughulika. Well, amini usiamini, baada ya mwaka mmoja na nusu niliweza kukosana na huyu mwanamke kwa sababu ya jambo dogo tu. Kilichonishangaza nikuwa  ile meseji ambayo nilimtumia mwaka na unusu iliyopita kumbe bado alikuwa nayo. Mwanzo alikuwa ameisave katika sehemu maalum k...

Mambo Ya Kufanya Na Kuepuka Ukipata Boyfriend Mpya

Image
  Kuingia katika mahusiano si jambo rahisi. Na sasa kwa kuwa umepata boyfriend mpya, si jambo zuri kuharibu kila kitu kwa wakati mmoja. Lakini kwa kuwa Nesi Mapenzi iko hapa, naamini kuwa hutakuwa na changamoto zozote ambazo zinaweza kukukumba. Kuwa na boyfriend mpya kuna raha zake. Huwa ni raha tupu. Utakuwa na muda mwingi wa kuweza kujuana na yeye na kila kitu kipya kumhusu. Na iwapo utagundua kuwa unampenda basi utataka kuishi na yeye kwa muda mrefu. Mambo ya kufanya ukipata mwanaume ama boyfriend mpya Kwa kawaida huwa tunapenda kuyafanya mahusiano yetu mapya kama ni mayai, tunaogopa yasije yakavunjika. Lakini ukweli ni kuwa ukiwa katika mahusiano mapya hupaswi kubadilika na kutatiza maisha yako ya kawaida. Wengi wetu wakiingia katika mahusiano mapya wanaogopa kuongea ama kufanya mambo ambayo wamezoea. Huwa wanaogopa kuwa wanaweza kuvunja mahusiano. Lakini ukibadilisha maisha yako kuna furaha gani ndani yake? Halafu pia kama hutakuwa na uwezo wa kuwa huru katika mahusiano mapya ...

SMS Ambazo Mwanamke Hapaswi Kumtumia Mwanaume Yeyote

Image
  Wanaume hupenda sana kuwasiliana na wanawake kupitia kwa SMS na njia nyingine za mitandao. Wanaweza kukusumbua siku nzima na SMS hizi. Halafu pindi ukianza kuongea na wao wanaweza kuja na mitindo mingine ya jumbe ambazo zinakuamuru ufanye jambo flani ama kutaka uwaonyeshe kitu flani. Ijapokuwa unaweza kuona kuwa ni mbinu nzuri ya kuwasiliana nao, wakati mwingine ni tabia mbaya. Unaweza ukamtumia mwanaume kitu flani na mwishowe akakudhalilisha ama kukushusha hadhi. So kama mwanamke, unapaswa kuweka mipaka kwa kile ambacho utamtumia mwanaume. Leo tumekuja na mambo ambayo hupaswi kumtumia mwanaume yeyote wakati wowote ule SMS unazopaswa kuepuka kumtumia mwanaume. #1 Picha za uchi. Hapa ni moja kwa moja. Usijaribu kumtumia mwanaume yeyote picha zako za uchi. Hata kama atatumia mbinu yeyote usikubali. Kutuma picha za uchi kwa mwanaume kuna madhara makubwa sana. Ukikosana na yeye anaweza kuzisambaza kwa mitandao na aibu ukurudie wewe. #2 Uongo. Usitumie uongo wowote kuteka atenshen ya ...