Posts

Showing posts with the label BIASHARA

BoT yaondoa hofu uhaba fedha za kigeni

Image
  PICHA: RENATHA MSUNGU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma jana, kuhusu asilimia sita ya riba ya BoT. BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewaondoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa fedha za kigeni huku ikisema imeimarika katika kipindi cha Julai hadi Septemba, mwaka huu. Imesema kuimarika huko kulikwenda sambamba na msimu wa shughuli za utalii na mauzo ya mazao ya kilimo na biashara nje ya nchi. Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, alisema jana jijini hapa kuwa kutokana na mwenendo huo, kasi ya kuporomoka kwa thamani ya shilingi ilipungua hadi kufikia asilimia 10.1 kwa mwaka unaoishia Septemba 2024, kutoka asilimia 12.5 kwa mwaka ulioshia Juni 2024,” alisema. Alibainisha kuwa akiba ya fedha za kigeni iliongezeka kufikia dola za Marekani milioni 5,413.6 mwishoni mwa Septemba kutoka dola za Marekani milioni 5,345.5  Juni, mwaka huu na kwamba kiasi hicho kinatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi...