HAWA HAPA WAZEE 8 WATAKAOSIMAMIA UCHAGUZI CHADEMA KITAIFA(MBOWE VS TUNDU LISSU)
Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika ametangaza kamati ya wazee wanane wastaafu ambao ni wanachama wa chama hicho, wenye jukumu la kusimamia mikutano ya kitaifa ya uchaguzi wa 2025.
Taarifa hiyo imeandikwa na John Mnyika kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X , ikiwataja wazee hao kuwa ni
- Ahmed Rashid
- Alfred Kinyondo
- Profesa Azaveli Rwaitama
- Wakili Edson Mbogoro
- Francis Mushi
- Lumuli Kasyupa
- Profesa Raymond Mosha
- Ruth Mollel.
Taarifa hiyo imesema uteuzi wa wazee hao umefanywa na kamati kuu katika kikao cha January 11,2025 kwa kuzingatia kanuni za chama kifungu cha 7.3.1.
Chanzo: upendo media
Comments
Post a Comment