Wawili wathibitika kuwa na ugonjwa wa mpox

Picha: Mtandao
ugonjwa wa mpox.
Wizara ya Afya imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa Mpox nchini, ambapo hadi sasa watu wawili wameugua, mmoja wao akiwa dereva wa magari ya mizigo aliyetoka nchi jirani kuelekea Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Jenister Mhagama, kupitia mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa, walipokea taarifa za wagonjwa wenye vipele usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili, pamoja na homa, maumivu ya kichwa, vidonda kooni na maumivu ya misuli.
Baada ya uchunguzi wa sampuli katika Maabara ya Taifa, Machi 9 mwaka huu, vipimo vilithibitisha maambukizi ya Mpox.
Comments
Post a Comment