Miaka mitano ya Covid-19: Fahamu nchi ambazo hazikufungia watu ndani



 Mnamo Machi 2020, mamilioni ya watu duniani walijikuta wamefungiwa majumbani mwao huku Covid-19 ikienea kwa kasi kubwa.

Nchi kadhaa hazikuweka vizuizi, hivyo je, maamuzi yao yalikuwa sahihi?

Mnamo Machi 2020, mamilioni ya watu walitumia madirisha yao kuchungulia nje.

Ghafla walijikuta wamefungiwa majumbani mwao, maisha yao yabadilika kwa haraka hadi kuwa ndani ya kuta nne na skrini za kompyuta.

Katika mataifa mengi, viongozi wa kitaifa walionekana kwenye televisheni wakihimiza watu kusalia makwao iipokuwa tu –wakati wa kununua bidhaa muhimu au kwa mazoezi ya kila siku.

Ilikuwa ni juhudi ya mwisho ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya kutisha ambavyo tayari vilikuwa vimeua maelfu ya watu duniani kote.

London, Tony Beckingham na mpenzi wake walifanya mazoezi yao ya kila siku wakiendesha baiskeli hadi katikati ya jiji jioni moja.

"Tulifikiri mazingira yatakuwa yakufurahisha kuona hakuna mtu," anasema.

Ilikuwa tofauti.

Maeneo waliyoyajua vizuri, kama Piccadilly Circus na Leicester Square, ambayo yalikuwa na watu wengi kila mara, yalikuwa kimya kwa hofu. "Yalikuwa ya kusikitisha – ," anasema Beckingham.

Kuzuia watu kuingia mitaani, maeneo ya biashara na biashara kulianza kwanza nchini China, ambapo Covid-19 ilianzia.



Amri za karantini zilifuatiwa kwa haraka katika nchi nyingine baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza janga mnamo Machi 11, 2020.

Hakuna wakati mwingine katika historia ya binadamu ambapo watu walikumbana na vizuizi kama hivi kwa kiwango kama hiki.

Lakini baadhi ya nchi zilifanya mambo tofauti. Sweden, Taiwan, Uruguay, Iceland na nyingine chache hazikufunga maeneo ambayo shughuli za watu, kama vile maagizo ya kisheria ya kukaa nyumbani ambayo yalitumika katika maeneo mengine.

Nchi hizo badala yake zilichagua hatua nyingine, kama vile vizuizi vya mikusanyiko mikubwa ya watu, upimaji wa kina na kuwatenga watu waliothibitika kuambukizwa au vizuizi vya safari.

Miaka mitano baadaye, tafiti za kisayansi na data zimeongezeka, zikitoa tathmini ya kina na ya muda mrefu kuhusu usahihi wa nchi hizi katika kukataa hatua hii kali zaidi ya afya ya umma.

...

Chanzo cha picha,Alamy

Maelezo ya picha,Mabilioni ya watu duniani kote yalikumbwa na kipindi cha upweke kufuatia hatua za kufungwa zilizowekwa awali kukabiliana na janga la Covid-19.

Jiji la Gothenburg nchini Sweden ni pepo kwa wapenda mbwa, anasema msimamizi wa rasilimali watu na mwandishi wa blogu, Anna Mc Manus, "Tuna jiji ambalo linapenda mbwa sana hapa," anasema.

Wakati nchi mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na majirani wa Sweden, Norway, Finland na Denmark, zilipoanza kuweka vizuizi vya kitaifa mnamo Machi 2020, Mc Manus alijua kuwa serikali yake ilikuwa imeamua kuepuka mwelekeo huo.

Alisikia namna wamiliki wa mbwa katika baadhi ya mataifa walivyoshindwa hata kuwapeleka wanyama wao matembezini kutokana na sheria za kutoka nje.

Afrika Kusini ilikuwa moja ya nchi hizo. Hii ilimgusa Mc Manus kama jambo baya. Wakati huo, aliandika chapisho la blogu alilosema, "Ninaamini kuwa serikali yangu inatekeleza hatua kwa njia salama na sahihi."

Hata hivyo, alionyesha pia wasiwasi kwamba Wasweden wenzake hawakuwa wakifuata kila mara miongozo rasmi ya afya kuhusu kuepuka kukaribiana , kama vile kuzuia idadi ya watu wanaoweza kukutana pamoja kwa kikundi.

Mc Manus anakumbuka mara kwa mara alipotembelea katika maeneo yenye vivutio, lakini pia anasema yeye na wenzake walivaa barakoa kila wakati ili kusaidia kuzuia maambukizi ya Covid-19 katika hospitali ya wanyama ambapo alifanya kazi mwaka 2020.

Zaidi ya hayo, yeye na mpenzi wake waliepuka mikahawa na kukutana na watu wengi.

Hata sasa, Mc Manus anasema hajui jinsi ya kuitafsiri mikakati rasmi ya Sweden.

"Nataka kuitegemea kwenye ukweli – kama vile ni watu wangapi walikufa," anasema. "Je, tusingeweza kuokoa watu wengi zaidi kama tungeweza kufunga maeneo?

Wanasayansi wamejaribu kujibu swali hilo. Ingeborg Forthun kutoka Taasisi ya Afya ya Umma ya Norway na watafiti kutoka mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Sweden walichapisha utafiti mnamo Mei 2024 ambao ulilinganisha vifo vya nchini Sweden, Norway, Denmark na Finland katika miaka ya kwanza ya janga hilo.

Ingawa Sweden iliepuka udhibiti mkali wa serikali, badala yake ikitegemea mabadiliko ya hiari ya tabia za raia wake, mataifa mengine manne yalitekeleza vizuizi vikali katika hatua za awali za janga hilo.

Norway, Finland na Denmark zilifunga shule na sehemu nyingi za shughuli za umma huku pia zikiwataka watu kufanyia kazi nyumbani, lakini waliepuka kuwafunga watu majumbani mwao kama ilivyofanyika katika nchi nyingine kama vile Uingereza.

Comments

Popular posts from this blog

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.