BONDIA HASSAN MGAYA AFARIKI BAADA YA KUPIGWA "TKO"

 



Bondia Hassan Mgaya amefariki dunia baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi sita lililofanyika usiku wa Desemba 28, 2024 ukumbi wa Dunia ndogo Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam.
Mgaya alicheza pambano hilo ambalo halikua la ubingwa na kupigwa TKO katika raundi ya sita dhidi ya aliyekua mpinzani wake Paulo Elias.
Inaelezwa kuwa Mgaya alipigwa na kwenda chini kisha mwamuzi akamhesabia na baada ya mwamuzi kumaliza kuhesabu marehemu akatembea hatua kadhaa hapohapo ulingoni kisha akaanguka na kuzimia.
Baada ya kuzimia marehemu akapewa huduma ya kwanza kutoka kwa madakatari waliokuwepo kwenye pambano na akazinduka kisha akapelekwa hospitali ya Sinza kwa ajili ya matibabu, Alipofikishwa hospitali ya Sinza akapatiwa rufaa ya kupelekwa hospital ya Mwananyamala na ndipo umauti ulipomkuta.
Kwa upande wake, bondia Cosmas Cheka kutoka chama cha mabondia nchini, amesema kuwa wapo mbioni kuandaa utaratibu wa kumsimamisha muandaaji wa pambano hilo Haji Ngoswe kwa kutoonyesha ushirikiano kwa bondia aliyefariki.
CHANZO: East african news

Comments

Popular posts from this blog

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.