NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka Watanzania kuanza kubadili mtazamo na kuziona taka kama fursa ya kuzirejeleza na kupata bidhaa mbalimbali na kujikomboa kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa jana, jijini Dar es Salaam na Meneja Utekelezaji wa Sheria wa baraza hilo, Amina Kibola, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amezungumza wakati akizungumzia siku ya kimataifa ya Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Taka, ambayo huadhimishwa kila Machi 30 kila mwaka. Anasema hata kauli mbiu ya mwaka huu, inaweka msisitizo wa kuwa taka si uchafu bali ni malighafi yenye thamani, endapo itasimamiwa na kutumika vyema. Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Amina Kibola, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kibola amesema siku hiyo ilianzishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 2022, ili kukuza mifumo endelevu ya matumizi na uzalishaji na kuongeza uelewa kuhusu udhibiti wa taka. Anasema siku hiyo pia ilianzishwa kwa len...