AINA 6 ZA MABOSI WAKOROFI NA JINSI YA KUKABILIANA NAO....
i. Wanafuatilia Kila Kitu
ii. Wanaoamini Katika Mawazo Yao Tu!
iii. Wanakuchukia Bila Kujua Sababu
iv. Wanaogopa Uwezo Wako
v. Wanaokupelekesha
vi. Wanaoamini Katika Mawazo Yao Tu!
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Nne Ya Mabosi
- Wanaogopa Uwezo Wako
Aina wako mabosi ambao huwa wamejaa hofu kubwa sana ya kupoteza nafasi yao (insecures bosses).
Na kwa sababu hiyo kila aliyeko chini yao ambaye anaonekana ni tishio kwa nafasi yao wataanza kumpiga vita kwa nguvu sana.
Mara nyingi sana mabosi wa namna hii utakuta uwezo wao ni mdogo kuliko nafasi waliyonayo.
Mara nyingi unakuta wamepata nafasi hizo kwa mbinu fulani.
Kujuana ama kupiga majungu wale ambao walikuwepo kabla yao.
Wakati wowote ule wakiona wewe unaanza kuonesha uwezo mkubwa ambao una hatarisha nafasi yao wataanza kukufanyia visa.
Na kukupiga vita ambayo inaweza hata kukuondoa kazini.
Kwa ufupi ni kuwa mabosi hawa huwachukia sana watu ambao wenye uwezo mkubwa.
Na wanapenda kukaa na watu ambao wana uwezo mdogo tu.
Kila wakati watakuwa wanafanya bidii ya kufanya usionekane na wengine na uwezo wako usijulikane kabisa.
Mabosi hawa ikitokea nafasi unayostahili kwenda kwenye mkutano, semina, kusoma ama kusafiri...
...na akahisi kwa kwenda kwako kutafanya uwezo wako uonekane na kutishia nafasi yao.
Atafanya kila mbinu kuhakikisha kuwa hauendi kabisa.
Ni waoga mno wa kupoteza nafasi yao.
Kama unataka Kujifunza Zaidi Mbinu Za Kuongeza THAMANI Yako Eneo la KAZI, Nashauri Usome eBook yangu ya UFANISI KAZINI.
CHANZO:JOELNANAUKA
Comments
Post a Comment