Nawanda afunguka magumu aliyopitia katika kesi ya ulawiti
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Nawanda amezungumza kwa mara nyingine baada ya kushinda kesi ya ulawiti, akisimulia magumu aliyopitia kipindi chote cha kesi hiyo. Dk. Nawanda alieleza hayo juzi wakati wa misa ya kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan na kumkumbuka baba mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa iliyofanyika katika mtaa wa Nyakabindi, mjini Bariadi. Alisema kuwa kipindi cha kesi yake kilimfundisha thamani ya kuishi vizuri na watu, akitoa shukrani kwa wananchi wa Simiyu kwa madai walionesha mapenzi makubwa na walimwombea kwa bidii. "Niwashukuru wananchi kwa dua na maombi yenu ambayo mlikuwa mkiniombea wakati ninapitia kipindi kigumu sana ambacho pia nilihitaji uwapo wa Mungu. Kwa hakika Mungu anampa mtihani mtu anayempenda," alisema Dk. Nawanda. Alisema kuwa wakati wowote Mungu hawezi kumpa mtihani mja wake ambao hawezi kuuhimili na kuwa alipewa mtihani huo akijua kuwa atauhimili. "Pia alijua nina watu na watu n...