Mwanasheria Mkuu mstaafu Jaji Werema afariki dunia, kuzikwa Januari 4 Butiama.

 


Aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali (AG mstaafu), Jaji Fredrick Werema amefariki dunia katika hospitali ya taifa muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na katibu wa halmashauri ya walei, parokia ya mtakatifu Martha Jimbo kuu la katoliki Dar es salaam, Salome Ntaro.

Kwa mujibu wa taarifa Jaji werema amefariki dunia mchana wa tarehe 30, decemba 20245. 

Ratiba kamili iliyotolewa na Familia yake ambayo imeeleza kuwa Januari 1,2025 ibada ya kumuombea marehemu itafanyika katika kanisa la mtakatifu Martha, mikocheni jijini Dar es salaam saa 9 alasiri.

Aidha, Ijumaa January 3, 2025 baada ya taratibu za kiserikali mwili utaondoka uwanja wa ndege kuelekea Butiama.


Chanzo: mwananchi.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.