Mwalimu Mkuu akamatwa tuhuma za kubaka mwanafunzi Kilosa
Mkuu wa Shule ya Sekondari Zombo, wilayani Kilosa, Mwalimu Mkame Living Mwaisumo (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama , amesema tukio hilo lilitokea Machi 19, 2025 , ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu, ambako mwanafunzi huyo alikuwa ameagizwa kupeleka mwongozo wa somo (lesson plan). Kamanda Mkama alieleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa tukio hilo limetokana na mmomonyoko wa maadili , huku uchunguzi wa kina ukiendelea ili kukamilisha hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa. DEREVA ALIYEIBA MAFUTA NA KULICHOMA LORI AKAMATWA Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi limemkamata Abubakar Adam Mwichangwe (29) , mkazi wa Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam , aliyekuwa akisakwa kwa tuhuma za wizi wa mafuta ya Dizeli lita 35,700 na kuchoma lori alilokuwa akiendesha ili kuonekana kama ajali. Kamanda Mkama amesema kuwa mtuhumiw...