UTEUZI:Rais Samia ateua viongozi wapya,,,,
Dk. Leonard Douglas Akwhilapo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Dkt. Akwhilapo, ambaye ni Katibu Mkuu Mstaafu, anachukua nafasi ya Prof. Penina Mlama aliyemaliza muda wake. Prof. Zacharia Babuu Mganilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Prof. Mganilwa, Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), anachukua nafasi ya Dk. Naomi Katunzi aliyemaliza muda wake. Dkt. Mwamini Madhebehi Tulli ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA). Dk. Tulli anahudumu kwa kipindi cha pili. Mhandisi Dk. Richard Joseph Masika ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Dk. Masika anachukua nafasi ya Prof. Henry Mahoo aliyemaliza muda wake. Balozi Salome Thaddaus Sijaona ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU). Balozi Sijaona ameteuliwa kwa kipindi cha pili. Prof. Joseph Nicolao...