Maseneta nchini Kenya wamuondoa Naibu wa rais Gachagua.

Maseneta wa Kenya wamepiga kura ya kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua ofisini licha ya kushindwa kutoa ushahidi wake katika kesi ya kumuondoa madarakani baada ya wakili wake kusema kuwa amepelekwa hospitalini.

Katika moja ya siku za kushangaza katika historia ya hivi majuzi ya kisiasa nchini Kenya, Gachagua alipaswa kufika katika Seneti baada ya chakula cha mchana kujitetea, siku moja baada ya kukanusha mashtaka 11.

Hata hivyo, Gachagua, almaarufu Riggy G, hakufika na wakili wake akaomba kuahirishwa akisema mteja wake alikuwa akisumbuliwa na 'maumivu ya kifua' na alikuwa akitibiwa na madaktari katika Hospitali ya The Karen.

Hata hivyo baada ya muda wa saa mbili kutoka saa tisa mchana hadi saa kumi na moja jioni Gachagua hakuweza kufika bungeni 

Mnamo Alhamisi jioni, theluthi mbili ya maseneta 67 waliohitajika walipiga kura ya kumtimua madarakani kwa tuhuma zinazojumuisha ufisadi, kuchochea migawanyiko ya kikabila na kuihujumu serikali.

Maseneta walipiga kura kwa wingi kumtia hatiani katika kura ya kwanza - kiasi cha kutosha kwake kuondolewa afisini.

Haya yanajiri miaka miwili tu baada ya Ruto na Gachgua kuchaguliwa kwa tiketi ya pamoja.

Kura hiyo inafikisha tamati ya mzozo wa miezi kadhaa katika ngazi ya juu ya serikali na kumpa fursa Ruto kujikita mamlakani.

Mzozo huo uliibuka mwezi Juni ambapo Gachagua, kwa kitendo kinachoonekana kumhujumu rais, alimlaumu mkuu wa shirika la ujasusi kwa kutomfahamisha Ruto na serikali ipasavyo kuhusu ukubwa wa maandamano ya kupinga nyongeza ya ushuru ambayo haikupendwa na watu wengi.

Katika pigo kubwa kwa mamlaka yake, Ruto alikuwa amelazimika kuondoa mapendekezo hayo ya ushuru. Alifuta baraza lake la mawaziri na kuleta wanachama wa upinzani kwenye serikali yake.

Ruto hajazungumzia tuhuma dhidi ya naibu wake.

Mwanzoni mwa kesi hiyo, mmoja wa mawakili wa Gachagua, Elisha Ongoya, alisema madai yote ni "ya uwongo, kejeli au aibu" .

Kabla ya kura hiyo, Gachagua alikuwa amesema angepinga uamuzi huo iwapo utapitishwa.

Daktari mmoja amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema Gachagua mwenye umri wa miaka 59 alienda hospitalini akiwa na tatizo la moyo, lakini alikuwa ametulia na anafanyiwa vipimo.

Vyombo vya habari vya Kenya tayari vimekuwa vikiripoti kuhusu uwezekano wa kubadilishwa kwake, huku watu wanne wakitajwa kama wanaowezwa kuteuliwa kuchukua wadhifa huo.

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.