Elon Musk Apagawishwa Na Uapisho Wa Trump, Sasa Ndoto Yake Ya Kupeleka Mtu Sayari Ya Mars Kutimia

 


Bilionea mkubwa duniani na mwanzilishi wa Kampuni ya SpaceX, Elon Musk ambaye pia ni swahiba mkubwa wa Rais Donald Trump wa Marekani, hapo jana alikuwa ni kama amepagawa kwa furaha wakati wa uapisho wa Trump.

Alipopewa nafasi ya kupanda jukwaani kwenye Ukumbi wa Capital One jijini Washington, Musk akiwa ni mwenye furaha kupitiliza, alifanya manjonjo mengi kwa furaha kabla ya kuanza kuzungumza.

Huku akishangiliwa kwa nguvu, Elon alinyanyua mikono yake juu kwa furaha huku akiutaja ushindi huo kuwa hatua muhimu kwa Marekani.

Alionesha matumaini makubwa juu ya mustakabali wa maendeleo makubwa hususan kwenye teknolojia ya roketi na anga za mbali.

“Hivi mnajua ni raha kiasi gani kuchomeka bendera ya Marekani katika sayari nyingine kwa mara ya kwanza?” alisema.

Musk alisisitiza ahadi ya Trump ya kuweka bendera ya Marekani kwenye Sayari ya Mars, akisema:

“Hii ni hatua inayohitajika sana kwa ndoto yetu ya kufanikisha utafiti wa anga za mbali.”

Kwa Musk, kuapishwa kwa Trump ilikuwa ni zaidi ya ushindi wa kisiasa – lilikuwa tangazo la mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia, tasnia ambayo amebobea.


CHANZO:GLOBALPUBLISHERS

Comments

Popular posts from this blog

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.