Posts

Showing posts from January, 2025

MBOSSO Kuondoka WCB- WASAFI

Image
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  @OfficialBabaLevo  kupitia ukurasa wake wa Instagram, imebainika kuwa msanii  @Mbosso_  amepewa uhuru wa kuondoka  @WCB_Wasafi  bila kulipa gharama yoyote. Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na heshima kubwa ambayo Mbosso ameonyesha kwa  @DiamondPlatnumz  na viongozi wa WCB. Diamond ameamua kumsamehe malipo yote yanayohusiana na kuondoka kwake, hivyo kumpa nafasi ya kujitafutia mafanikio mapya kama msanii huru. Baba Levo alidokeza kuwa WCB inapanga kusaini wasanii wapya tisa mwaka huu 2025

Mkuu wa Jeshi la Afrika Kusini amjibu Rais Kagame

Image
  Picha:Mtandao Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini (SANDF), Jenerali Rudzani Maphwanya. Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini (SANDF), Jenerali Rudzani Maphwanya, amejibu kauli ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuhusu mchango wa vikosi vya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akisisitiza kuwa jeshi la kikanda limeisababishia hasara kubwa M23 katika mapambano ya hivi karibuni. Jenerali Maphwanya amesema kuwa Kikosi cha Kulinda Amani cha Kikanda nchini  DRC  ( SAMIDRC ), kinachojumuisha vikosi vya jeshi kutoka  Afrika Kusini, Malawi,  na  Tanzania , kimefanikiwa kuwadhibiti waasi wa  M23 , ambao wamekuwa wakisababisha machafuko mashariki mwa nchi hiyo. Katika taarifa yake leo, Maphwanya alieleza kuwa waasi wa M23 wanadaiwa kupata mafunzo na kuungwa mkono na Serikali ya  Rwanda , ambayo ni jirani wa DRC. "Tishio kuu katika eneo hili linatokana na kundi la waasi ambalo linadaiwa kuwa na silaha, ku...

CLEMENT MZIZE NA STEPHEN AZIZI K HAOOO AL ITTHAD

Image
  Klabu ya Al Itthad ya nchini Libya imeonesha nia ya dhati ya kupata huduma za wachezaji wawili tegemeo wa Yanga CLEMENT MZIZE NA STEPHEN AZIZI K ,kulingana na dau ambalo inasemekana wameliweka ili kupata saini za wachezaji hao ifikapo june 2025,, Kama ambavyo ananukuliwa mwandishi maarufu wa habari za michezo nchini Ghana MICKJR "Al Ittihad has reached an agreement with Yanga to transfer Clement Mzize and Stéphane Aziz to the Libyan giants. Understand; It was a 𝐜𝐫𝐚𝐳𝐲 offer that’s very difficult to turn down by the reigning champions in Tanzania. Club to club agreement is done but the move can only happen in June — the wish of Yanga. Ittihad now needs to negotiate with both players for salary structure, bonuses and working conditions. One player is keen on the move, but the other one is reluctant. More updates to come soon."

Rais wa Rwanda Paul Kagame kutoa onyo kali kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Image
  Mahusiano kati ya Rwanda na Afrika Kusini yanaweza kuwa si mazuri kwa sasa hii ni baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kutoa onyo kali kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, akisema kwamba Rwanda imejiandaa kwa lolote iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo. Taarifa ya Rais Kagame ilikuwa inajibu maoni ya Rais Ramaphosa juu ya jukumu la Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda na Kikundi cha Waasi cha M23 katika mapigano yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Jibu la Rais Paul Kagame kwa Cyril Ramaphosa liliashiria mzozo mbaya wa kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Rwanda. Katika taarifa iliyo na maneno makali akimjibu moja kwa moja Cyril Ramaphosa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Kagame alimshtumu Rais wa Afrika Kusini kwa kupotosha mazungumzo ya faragha juu ya hali tete mashariki mwa DRC. Kiongozi huyo wa Rwanda pia amesema Rais Ramaphosa alikuwa hajaonya Rwanda juu ya shughuli zake za kijeshi DRC lakini badala yake alikuwa ameomba msaada wa vifaa, pamoja na umeme,...

MBOWE KUTOTOKEA WAKATI WA MAKABIDHIANO MAKABIDHIANO, MNYIKA ATOA MAJIBU

Image
  Kuhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutoonekana wakati wa makabidhiano ya ofisi, Katibu mkuu wa CHADEMA  John Mnyika alisema katiba ya chama hicho inaruhusu Katibu Mkuu kusimamia zoezi hilo na kwamba hakuna shida kama watu wanavyodhani.

Lissu ataka Bunge la dharura kufumua sheria za uchaguzi,.

Image
  Home Habari Biashara Michezo Burudani Makala Safu Maoni Maktaba EDITIONS The Guardian Nipash Vilevile, chama hicho kimetoa mapendekezo matatu kwa serikali kukabili mabadiliko ya kisera kwenye misaada katika sekta ya afya yaliyofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump. Lissu alisisitiza msimamo huo jana mkoani Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi katika makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, wilayani Kinondoni. Lissu alisema kuna Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, lakini kwao CHADEMA, kama hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lakini haina maana watasusia uchaguzi. "Tusijaribu kuitanua lugha kuliko maana yake ya kawaida, hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi. Lazima tuzungumze hayo mambo mawili tuone tunawezaje tukaenda nayo mbele aidha kwa pamoja au kuamua lipi muhimu. "Sasa hilo sitaki nizungumze hapa, zaidi tunakwenda kujifungia kisha tutaamua kwa pamoja ili uwe uamuzi wa chama na si wangu peke yangu. Tutakwenda kuonana na marafiki zetu duniani tuwaambie msim...