Posts

Showing posts from September, 2024

MAGAZETI YA LEO TAREHE 01-10-2024

Image
                     

Elie Mpanzu atambulishwa Simba

Image
 Karibu simba Mpanzu Elie 🦁. Simba Sports Club rasmi wamemtambulisha usajili wa Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo Elie Mpanzu Kibisawala (22)🇨🇩  kwa mkataba wa miaka miwili.

‘Mwishowe, nimeshinda,’ mfungwa aliyetumikia kifungo cha muda mrefu zaidi duniani azungumza

Image
  ‘Mwishowe, nimeshinda,’ mfungwa aliyetumikia kifungo cha muda mrefu zaidi duniani azungumza Mfungwa aliyehukumiwa kifo kwa muda mrefu zaidi duniani aliwashukuru wafuasi wake kwa kumsaidia kupata “ushindi kamili” baada ya mahakama ya Japan wiki iliyopita kubatilisha hukumu yake ya mauaji ya miongo kadhaa. Baada ya vita vya muda mrefu vya kudai haki vilivyoongozwa na dada yake, Iwao Hakamada mwenye umri wa miaka 88 siku ya Alhamisi alitangazwa kuwa hana hatia ya mauaji ya mara nne ambayo alitumia miaka 46 kwenye hukumu ya kifo. “Hatimaye nimepata ushindi kamili na kamili,” bondia huyo wa zamani aliliambia kundi la wafuasi Jumapili huko Shizuoka, eneo la kusini magharibi mwa Tokyo ambapo uamuzi huo ulitolewa. “Sikuweza kusubiri tena” kusikia uamuzi wa kutokuwa na hatia, alisema Hakamada anayetabasamu, akivaa kofia ya kijani. “Asante sana,” akaongeza, akiandamana na dada yake Hideko mwenye umri wa miaka 91 kwenye mkutano huo, ambao ulionyeshwa kwenye televisheni ya Japani. Japani na ...

Utekelezaji miradi ya maendeleo uzingatie vipaumbele vya wananchi- Kapinga

Image
  Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Judith Kapinga amesema dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanashirikishwa katika kufanya maamuzi ya maendeleo katika maeneo yao.  Aidha, Viongozi katika ngazi mbalimbali wahakikishe maamuzi hayo yanazingatia  mipango na programu zinazoakisi hali halisi ya wananchi, mahitaji yao pamoja na  vipaumbele. Kapinga amesema hayo leo Septemba 30, 2024 wakati akifungua Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi, Watendaji na Wadau wa Wilaya ya Mbinga. Ameongeza kuwa, Serikali inataka kuona wananchi wanasimamia maendeleo yao kwa kufanya maamuzi na kuweza kufuatilia na kusimamia utekelezaji wake kwa kutumia vigezo vya kitakwimu. Amesema  Sensa za Watu na Makazi hufanyika kwa lengo la kupata takwimu za msingi za watu na hali ya makazi yao ili kusaidia kutunga Sera, kupanga na kufuatilia mipango ya maendeleo ya kimkakati inayolenga kukuza uchumi wa nchi na watu wake. ...

"Waliotumwa na afande" wahukumiwa kifungo cha maisha jela

Image
    Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam. Katika kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 iliyokuwa inawakabili washtakiwa hao akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba. Kesi hiyo maarufu ‘Waliotumwa na Afande’ imesikilizwa faragha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ambapo upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya Washtakiwa. Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024. Hata hivyo Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya Shilingi milioni 1. Washtakiwa walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza August 19, 2024 na kusom...

Amuua mwenzake kisa Sh 200

Image
  Mwanaume mmoja aliyefahamika Kwa jina la Kulwa Bosco (27) maarufu Kwa Jin la Rasta anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linàmshikilia kulwa Bosco mkazi wa Kijiji cha Sinyaulime Tarafa ya Ngeregere Wilaya na Mkoa Morogoro kwa tuhuma za kumuua Hussein Nyabu (35)kwa kumchoma na kitu chenye ncha Kali kifuani na kusababisha kifo chake.   Akitoa taarifa yake kwa waandishi wa Habari kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema kuwa chanzo Cha tukio hilo ni ugomvi uliosababishwa na mtuhumiwa na marehemu kugombea Shilingi 200 wakati wakicheza mchezo wa pool Table ndipo mtuhumiwa alitoa kitu chenye ncha Kali na kumchoma marehemu   Tukio hili limetokea septemba 29 majira ya saa moja jioni katika kitongoji Cha Ngerengere Kaskazini Kata ya Ngerengere wilaya ya Morogoro vijijini katika baa moja maarufu kama maokoto   Jeshi la posili linawataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia Sheria Mkononi bali wajikite katika kufanya kazi za kujiingizia ...

Mnibake mimi na sio binti zangu' - vita vya kutisha vya Sudan

Image
  Sudan iko katika hali mbaya. Baada ya miezi 17 ya vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoiangamiza nchi hiyo, jeshi limefanya mashambulizi makubwa katika mji mkuu Khartoum, yakilenga maeneo yaliyo mikononi mwa mpinzani wake mkali, Kikosi cha RSF RSF iliteka sehemu kubwa ya Khartoum mwanzoni mwa mzozo, wakati jeshi linadhibiti mji pacha wa Omdurman, ng'ambo ya Mto Nile. Lakini bado kuna mahali ambapo watu wanaweza kuvuka kati ya pande hizo mbili. Wakati mmoja, nilikutana na kikundi cha wanawake ambao walikuwa wametembea kwa saa nne hadi sokoni katika eneo linalodhibitiwa na jeshi kwenye ukingo wa Omdurman, ambapo chakula ni cha bei nafuu. Wanawake hao walikuwa wametoka Dar es Salaam, eneo linaloshikiliwa na RSF. Waume zao walikuwa hawaondoki tena nyumbani, waliniambia, kwa sababu wapiganaji wa RSF waliwapiga, walichukua pesa zozote walizopata, au waliwaweka kizuizini na kudai malipo ya kuachiliwa kwao. “Tunavumilia ugumu huu kwa sababu tunataka kuwalisha watoto wetu. Tun...

MJITOKEZE KUJIANDIKISHA KWENYE ORODHA YA WAPIGAKURA WA SERIKALI ZA MITAA OKT. 11-20'

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wote wenye sifa kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga kura wa Serikali za Mitaa utakaofanyika nchi nzima Oktoba 11-20, 2024. Mhe. Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati alihutubia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa mkoani  Ruvuma katika mkutano uliofanyika viwanja vya Bandari ya Mbambabay. Amesema ili uwe mpigakura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ni lazima uwe umejiandikisha kwenye Orodha ya Wapigakura wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 11-20/10/2024 nchi nzima na uandikishaji utafanyika kwenye vijiji/vitongoji pamoja na mitaa. "Hivyo niwaombe wananchi wote wenye sifa muda ukifika mkajiandikishe, hili daftari la Kudumu la Wapigakura linaloendelea hivi sasa kwenye maeneo mbalimbali ni kwa ajili ya uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais utakaofanyika mwaka 2025 ila kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 mnatakiwa wote mkajiandikishe kwenye mitaa...

Watu 17 wauawa katika ufyatulianaji risasi Afrika Kusini

Image
  Watu kumi na saba wakiwemo wanawake 15 wameuawa katika ufyatulianaji wa risasi wakati wa mauaji yaliyotokea katika matukio mawili tofauti nchini Afrika Kusini. Polisi imesema mauaji hayo yalikitokea usiku wa kuamkia Jumamosi katika mji wa Lusikisiki, jimbo la Western Cape MATAN Brigedia Athlenda Mathe, msemaji wa polisi ya   Afrika Kusini  amesema msako unaendelea kuwatafuta washukiwa hao. Taarifa ya polisi imesema wanawake kumi na wawili na mwanaume mmoja waliuawa katika nyumba moja na wanawake watatu na mwanamume mwengine waliuawa katika nyumba nyingine. Muathiriwa mwengine mmoja amelazwa hospitalini akiwa kati hali mbaya. Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani. Na visa vya mauaji ya watu wengi vimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Huku wakati mwingine watu hulengwa wakiwa nyumbani mwao.