Posts

CHADEMA hatarini kufutiwa usajili

Image
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kipo katika hatari ya kufutiwa usajili iwapo kitaendelea na kuwatambua viongozi waliovuliwa uongozi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Katika barua ya Msajili iliyotoa taarifa kwa ofisi hiyo imeeleza kuwa inayo mamlaka ya kukifutia usajili chama hicho endapo kitaendelea kuwatambua viongozi hao. “Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inapenda kuwakumbusha wanachama na viongozi wa CHADEMA kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria ya Vyama vya Siasa Msajili anayo mamlaka ya kusimamisha usajili wa chama hicho” imesema sehemu ya barua ya Msajili. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imeendelea na msisitizo wake wa kutoitambua Sekretarieti ya uongozi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayomjumuisha Katibu Mkuu wake John Mnyika. Sekretarieti hiyo ya CHADEMA iliteuliwa Januari 22 mwaka huu kwenye Baraza Kuu la chama hicho baada ya kupatikana kwa uongozi mpya unaoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa, Tundu Lissu. cha...

Kiongozi Mbio za Mwenge asisitiza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Image
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ussi, ametoa wito kwa wananchi kuendeleza amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Ussi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika Wilaya ya Rufiji wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusambaza ujumbe wa kitaifa wa Mbio hizo. Aliwahimiza wananchi kuzingatia ujumbe wa mwaka huu unaosema: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu,” akisisitiza kuwa uchaguzi uwe huru, wa haki na wa kumalizika kwa amani kama ilivyopangwa na taifa. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), alisema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa chachu ya maendeleo nchini kwa kufika katika kila pembe ya Tanzania kukagua na kuchochea utekelezaji wa miradi inayogusa maisha ya wananchi. “Tu...

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO

Image
  Geofrey Kiliba, mwanafunzi wa Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwa mwaka wa uongozi 2025/2026, katika uchaguzi mkuu uliofanyika leo visiwani Zanzibar. Kiliba alipata ushindi huo mkubwa kwa kuungwa mkono na kura nyingi kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAHLISO, ambao wanawakilisha serikali za wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini. Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Kiliba aliwashukuru wajumbe kwa imani waliyoionesha kwake, na kuahidi kuwa kiongozi mwenye maadili, uwazi, ushirikiano na weledi katika kutekeleza majukumu yake. Aliahidi kujenga TAHLISO imara, yenye kusikiliza na kutetea maslahi ya wanafunzi kwa nguvu na hekima. “Nitakuwa kiongozi mwenye masikio makubwa na mdomo mdogo; niko tayari kusikiliza hoja na haja zenu. Sote tuna ndoto za kuwa viongozi, lakini leo naomba mtangulize maono ili nitimize ya kwetu sote,” alisema Kiliba kwa u...

Watia nia CHADEMA 55, waibuka na hoja tisa kuhusu ‘no reforms no election’

Image
Picha: Mtandao Ofisi ya CHADEMA. Watia nia 55 wa ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mwaka 2025, wakiwakilisha zaidi ya 200 walioonesha nia, akiwemo baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho, wameibuka na hoja tisa kuhusu msimamo wa chama huo wa kutoshiriki uchaguzi endapo hakutakuwa na mageuzi ya kisiasa ('No reforms, no election'). Kupitia waraka walioutuma Aprili 4, 2025 kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, watia nia hao wameeleza kuwa msimamo huo kwa sasa unakinzana na malengo yake ya awali. Wamedai kuwa haiwezekani kuzuia uchaguzi kwa kuwa nje ya mchakato huo, wakisema hatua hiyo inaweza kuchukuliwa kama kitendo cha jinai. Kwa mujibu wa waraka huo, njia pekee ya kuzuia uchaguzi isiyo huru ni kushiriki mchakato huo kwa kuingiza wagombea, ambao wanaweza kuhamasisha na kuongoza wananchi kuzuia uchaguzi katika maeneo mahsusi yenye viashiria vya hujuma, badala ya kuwa nje ya mchakato mzima. Hoja tisa kuu zilizowasilishwa: 1. ✍🏿 Mbinu ya Kuzuia Uchaguzi Kutoka ...

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza nafasi za kazi za watendaji wa uchaguzi Tanzania Zanzibar

Image
  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza nafasi za kazi za mratibu wa uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi na msimamizi msaidizi wa uchuguzi ngazi ya jimbo watakaosimamia Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara kwa upande wa Tanzania Zanzibar Kwa mujibu wa tangazo la Tume lililosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima, R. K, nafasi hizo ni kwa Unguja na Pemba na wanaotakiwa kuomba nafasi hizo ni raia wa Tanzania, watumishi wa umma na sifa nyingine zilizoainishwa kulingana na nafasi inayoombwa. Tangazo hilo limemtaka kila mwaombaji aainishe nafasi anayoiomba, akitaja wilaya au jimbo analotaka kufanyia kazi na aambatishe vyeti vya elimu pamoja na maelezo binafsi (CV) na maombi yatapokelewa kuanzia tarehe 3 Aprili, 2025 hadi tarehe 23 Aprili, 2025 saa 9:30 Alasiri. Maombi hayo yanatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Maisara kwa upande wa Unguja na Chakechake (Mtaa wa Miembeni) kwa upande wa Pemba kwa a...

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

Image
  BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka Watanzania kuanza kubadili mtazamo na kuziona taka kama fursa ya kuzirejeleza na kupata bidhaa mbalimbali na kujikomboa kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa jana, jijini Dar es Salaam na Meneja Utekelezaji wa Sheria wa baraza hilo, Amina Kibola, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amezungumza wakati akizungumzia siku ya kimataifa ya Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Taka, ambayo huadhimishwa kila Machi 30 kila mwaka. Anasema hata kauli mbiu ya mwaka huu, inaweka msisitizo wa kuwa taka si uchafu bali ni malighafi yenye thamani, endapo itasimamiwa na kutumika vyema. Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Amina Kibola, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kibola amesema siku hiyo  ilianzishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 2022, ili kukuza mifumo endelevu ya matumizi na uzalishaji na kuongeza uelewa kuhusu udhibiti wa taka. Anasema siku hiyo pia ilianzishwa kwa len...

AINA 6 ZA MABOSI WAKOROFI NA JINSI YA KUKABILIANA NAO....

Image
i. Wanafuatilia Kila Kitu ii. Wanaoamini Katika Mawazo Yao Tu! iii. Wanakuchukia Bila Kujua Sababu iv. Wanaogopa Uwezo Wako v. Wanaokupelekesha vi. Wanaoamini Katika Mawazo Yao Tu! Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Nne Ya Mabosi  - Wanaogopa Uwezo Wako  Aina wako mabosi ambao huwa wamejaa hofu kubwa sana ya kupoteza nafasi yao (insecures bosses). Na kwa sababu hiyo kila aliyeko chini yao ambaye anaonekana ni tishio kwa nafasi yao wataanza kumpiga vita kwa nguvu sana.  Mara nyingi sana mabosi wa namna hii utakuta uwezo wao ni mdogo kuliko nafasi waliyonayo.  Mara nyingi unakuta wamepata nafasi hizo kwa mbinu fulani. Kujuana ama kupiga majungu wale ambao walikuwepo kabla yao.  Wakati wowote ule wakiona wewe unaanza kuonesha uwezo mkubwa ambao una hatarisha nafasi yao wataanza kukufanyia visa. Na kukupiga vita ambayo inaweza hata kukuondoa kazini. Kwa ufupi ni kuwa mabosi hawa huwachukia sana watu ambao wenye uwezo mkubwa. Na wanapenda kukaa na watu ambao wan...