TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema imebaini uwepo wa changamoto kwa baadhi ya watu kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti wakati wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Dar es Salaam. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani, huku akibainisha hatua ambazo zinachukuliwa na tume hiyo baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika. Amesema baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika katika vituo, tume inachakata taarifa za watu wote walioandikishwa kupitia mfumo maalum wa alama za vidole ambao una uwezo wa kuwabaini wapiga kura wote waliojiandikisha zaidi ya mara moja. “Kingine tume hufanya zoezi la kulinganisha sura za watu wote walioko kwenda daftari lengo ni kubaini iwapo kuna waliojiandikisha zaidi ya mara moja. “Pia iwapo itabainika mtu amejiandikisha zaidi ya mara moja, jina na taarifa za mtu huyo, hufutwa na mfumo katika vituo vingine na kubakizwa katika kituo cha mwisho alichojiandikisha ...
Picha: Mpigapicha Wetu Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai Wanawake wawili wanaodhaniwa kuwa washirikina wamekamatwa alfajiri hii wakiwa watupu katika madhabahu ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. Tukio hili limeleta taharuki kubwa baada ya wanawake hao kudai walitumwa kuchukua ulimi wa marehemu aliyezikwa hivi karibuni katika makaburi ya usharika. Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na wanawake hao wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi. Mwinjilisti wa Usharika wa Nkwarungo, Jeremiah Nkya, alisema walinzi walikamata wanawake hao wakiwa na mabunda ya vitu visivyoeleweka. chanz:nipashe
Picha: Mpigapicha Wetu Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi OFISA Utumishi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Nicodemus Tindwa, amesema mchakato wa kuligawa Jiji hilo kuwa majimbo mawili ya uchaguzi umekamilika, baada ya wataalamu wa halmashauri kufanya tathmini na kubaini kuwa linakidhi vigezo vinavyotakiwa. Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Tindwa, amesema Jiji la Mbeya lina tarafa mbili, kata 36, mitaa 181, na lina ukubwa wa kilomita za mraba 258.8. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, linakadiriwa kuwa na wakazi 141,603. Kutokana na hali hiyo, Jiji la Mbeya litakuwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Mbeya Mjini na Jimbo la Uyole.
Comments
Post a Comment