Mtanzania ateuliwa bosi Umoja wa Afrika

 



  • Dk Rwegasha ambaye anatarajiwa kuanza kazi Februari mwaka huu amemshukuru Mungu kwa nafasi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa katika mchakato wa usaili.

Dar es Salaam. Tanzania imeendelea kung’ara katika nyanja za kimataifa baada ya Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk John Rwegasha kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Tiba, Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Dk Rwegasha ambaye anatarajiwa kuanza kazi Februari 2025 katika nafasi hiyo mpya amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa katika mchakato wa usaili.

Akiagana na Menejimenti ya MNH mwishoni mwa wiki hii, Dk Rwegasha amesema amefanikiwa kufaulu na kuteuliwa rasmi kati ya washindani wenzake kutoka mataifa saba ya Afrika.

Comments

Popular posts from this blog

Tume huru ya uchaguzi yabaini watu kujiandikisha zaidi ya mara moja

Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai

Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi