WABUNGE 19 WAJERUHIWA AJALI YA BASI LA SHABBY WAKIELEKEA KENYA

 



Habari zilizotufikia Matukio Daima media muda huu zinaeleza kuwa wabunge zaidi ya 50 waliokuwa wakisafiri kwa basi kutoka Dodoma kwenda Nchini Kenya kushiriki michezo wamepata ajali eneo la Mbande mkoani Dodoma.

Wabunge kadhaa wamepata majeraha ya Mwili kutokana na ajali hiyo .

Imeelezwa kuwa basi hilo la Bunge likiwa katika mwendo wa kawaida lilikutana na changamoto ya gari jingine lililokuwa limeangusha mizigo barabarani na wakati dereva akijaribu kukwepa mizigo hiyo ndipo basi hilo lilipoacha njia na kuingia Porini.

Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Matukio Daima media kuwa miongoni mwa wabunge waliojeruhiwa ni pamoja na mbunge wa Kalenga Jackson Kiswaga ,Mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu,mbunge wa Viti maalum chadema Grace Tendega 

Shuhuda huyo alisema  basi lililopata ajali  ni  moja kati ya mabasi manne ya Shabiby yaliyokuwa  yanawasafisha kwenda kwenye mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki Mombasa Kenya, amesema kuwa ajali hiyo imetokea  leo alfajiri baada ya basi moja kudaiwa kugonga nyuma ya lori lililokuwa limesimama katika Barabara hiyo ya Morogoro - Dodoma.

"Tunashukuru Mungu wenzetu wamenusurika basi moja kati ya manne tuliyokuwa tunasafiria limepata ajali na baadhi ya wenzetu wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali za Uhuru na Benjamini Mkapa kwa ajili ya matibabu, hatujui hadi sasa wenzetu wanaendeleaje, nasi bado tupo eneo la ajali," amesema Mbunge huyo ambae hakutaka jina lake kuandikwa kwa kuwa si Msemaji wa bunge 


Msafara huo  ambao ulitakiwa kupitia Chalinze na Tanga kwenda Mombasa, umejumuisha wabunge na watumishi wa Bunge zaidi ya 120 wanaokwenda kushiriki michezo mbalimbali inayotarajia kuanza kesho Desemba 7 hadi Desemba 17 mwaka huu na kushirikisha timu za mabunge  ya Nchi 7 likiwemo Bunge la Afrika Mashariki.


chanzo:

Comments

Popular posts from this blog

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

APPLICATIONS hizi HAPA haziruhusiwi kutoa mikopo mtandaoni

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO