Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu azuiwa kugombea tena urais

 




Mahakama ya juu nchini Zambia imemzuia Rais wa zamani Edgar Lungu kugombea tena urais mwaka 2026.

Mahakama ya Kikatiba iliamua kwamba mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 68 tayari alikuwa ametumikia mihula miwili inayoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Lungu alichaguliwa kuwa rais kwa mara ya kwanza Januari 2015 kutumikia miezi 20 iliyosalia ya muhula wa mtangulizi wake.

Rais Michael Sata alifariki akiwa madarakani Oktoba 2014. Lungu alikuwa amedai kuwa hii isihesabiwe maana hakuhudumu kwa muhula mzima wa miaka mitano.

Lakini mahakama haikukubali, ikibadilisha maamuzi ya awali ambayo yalimruhusu kugombea miaka mitatu iliyopita aliposhindwa na Hakainde Hichilema.

"Bw Edgar Chagwa Lungu kwa hivyo amechaguliwa mara mbili na ameshikilia wadhifa wake mara mbili. [Katiba] inamfanya kutostahili kushiriki katika chaguzi zozote zijazo kama mgombea urais," mahakama iliamua

Comments

Popular posts from this blog

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

APPLICATIONS hizi HAPA haziruhusiwi kutoa mikopo mtandaoni

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO