Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 1,548

 



RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa msamaha kwa wafungwa 1,548 huku kati yao 22 wakiachiliwa huru.

Hatua hiyo ya Rais Samia ni kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania bara,  inayoadhimishwa kila mwaka, Desemba 9.

Taarifa iliyotolewa leo, Desemba 9, 2024 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, ilisema kwamba kati ya wafungwa hao walionufaika na msamaha, 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki.

“Rais ametumia Mamlaka aliyopewa chini ya lbara ya 45(1)(a) - (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa msamaha kwa wafungwa.”

Comments

Popular posts from this blog

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

APPLICATIONS hizi HAPA haziruhusiwi kutoa mikopo mtandaoni

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO