Mapacha Hussein, Hassan warejea nchini baada ya kutenganishwa Saudi Arabia

 







MAPACHA Hussein na Hassan Jumanne (3), waliokuwa wameungana wamerejea nchini, wakitokea nchi ya Saudi Arabia walikokaa kwa takribani mwaka mmoja, ili kuwatenganisha.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Rachel Mhavile, akizungumza na waandishi wa habari, punde baada ya watoto hao kuwasili kutoka Saudia Arabia, kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, leo, amesema;

"Ni furaha kwetu kama MNH kuwapokea tena mapacha hawa kutoka nchi ya Saudi Arabia, walikokaa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Wamerudi wametenganishwa na sasa mama ataweza kuwahudumia kirahisi."

Mama wa watoto hao, Hadija Shaban (24), amesema kwamba anaishukuru MNH, kwa kuwahudumia watoto wake hadi sasa na kwamba anawaomba wasamaria wema waendelee kumpa msaada wa hali na mali, ili ajikimu na awe na sehemu bora ya kuishi.

"Mimi ndio baba, mama...nawaomba wasamaria wema, Watanzania, waendelee kunisaidia, ili niwahudumie watoto hawa. Kwa sababu wanatakiwa kuwa na mahitaji ambayo ni ya msingi wote kwa pamoja," amesema.

Bingwa wa Upasuaji wa Watoto MNH, Dk. Zaitun Bokhary, amesema watoto hao wanaendele vizuri ikiwa ni miezi miwili tangu wafanyiwe upasuaji wa kuwatenganisha.


Comments

Popular posts from this blog

Tume huru ya uchaguzi yabaini watu kujiandikisha zaidi ya mara moja

Wanawake wawili wakamatwa wakiwa watupu katika Madhabahu ya KKKT Hai

Jiji la Mbeya kugawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi