Mahakama ya Ufaransa yampata na hatia mwandishi aliyepuuza mauaji ya kimbari ya Rwanda

 






Mwandishi wa kifaransa na Cameroon ,Charles Onana, amepatikana na hatia na mahakama ya Ufaransa kwa kupuuza mauaji ya kimbari ya Rwanda katika kitabu chake cha Rwanda,the Truth About Operation Turquoise.

Mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 60 ametozwa faini ya dola 8,900 na mchapishaji wake Damien Serieyx ameamriwa kulipa faini ya dola 5,260.87 .

Pia wanatakiwa kulipa dola 11,575 kama fidia kwa mashirika ya haki za binadamu.

Mahakama ilisema kuwa makala ya Onana yalikiuka sheria za Ufaransa zinazozuia kukanusha mauaji ya kimbari na kuchochea chuki.

Kitabu cha Onana,kilichochapishwa mwaka 2019,kilidai kuwa mauaji ya kimbari ya Rwanda ni ‘’hadaa’’ na kupinga kwamba serikali ya Hutu ilipanga mauaji ya kimbari.

Mahakama ilisema kitabu chake kilishangaza baada ya kupinga mauaji ya kimbari ya 1994 ambayo watu takribani laki nane wengi wao wakiwa watusi waliuawa.

Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe alikubaliana na hukumu hiyo akisema ilikuwa ‘’uamuzi muhimu’’. Hata hivyo Onana na mchapishaji wake wamelalamikia hukumu hiyo na wamekata rufaa

Comments

Popular posts from this blog

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.