MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida, Jackson Jingu, ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kushindwa vibaya na Diwani wa Kata ya Ntuntu wilayani Ikungi, Omari Mohamed Toto. Kutokana na hilo, Jingu ametangaza Uchaguzi Mkuu 2025 atawania ubunge katika Jimbo la Singida Magharibi. Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi mjini Singida ambao pia, ulihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, Jingu aliambulia kura 30 dhidi ya mpinzani wake, Toto aliyeibuka kidedea kwa kupata kura 52, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Wilson Luta aliyepata kura tano. Msimamizi wa uchaguzi huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Patrick Ole Sosopi, akitangaza matokeo hayo alisema nafasi ya Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Singida, aliyeshinda ni Samweli Maro kwa kupata kura 58 na hivyo kufanikiwa kutetea nafasi yake hiyo. Alisema nafasi Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Singida, ilichukuliwa na Joseph Salum huku uchaguzi wa nafasi Katib...