Sababu za kutaka kumuondoa madarakani naibu rais wa Kenya


.

Chanzo cha picha,X/Rigathi Gachagua

Maelezo ya picha,Naibu wa Rais Rigathi Gachagua
  • Author,

Wandani wa Rais wa Kenya William Ruto waliwasilisha hoja bungeni siku ya Jumanne ya kumshtaki Naibu Rais Rigathi Gachagua wakimtuhumu kwa kuchochea chuki za kikabila na kuidhoofisha serikali.

Tofauti kati ya rais Ruto na Gachagua zimeongezeka katika siku za hivi karibuni. Gachagua anasema ametengwa na amekanusha shutuma za washirika wa Ruto kwamba alihusika na maandamano ya kupinga serikali mapema mwaka huu.

Pia wanadai kwamba Gachagua amejihusisha na masuala ya ufisadi , kuihujumu serikali na kukukuza siasa za kikabila.

Raia Ruto alimchagua Gachagua kama naibu wake katika uchaguzi wa 2022 ambapo walimshinda aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali

Gachagua anatoka katika eneo la Mlima Kenya ambapo Rais Ruto alijipatia wingi wa kura ili kuibuka mshindi.

Tayari washirika wa kiongozi huyo wamefanya majaribio kadhaa ya kuzuia kura hiyo ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Wabunge wanaomuunga mkono rais Ruto wamesema kwamba wana zaidi ya idadi inayohitajika ya kumuondoa kiongozi huyo serikalini.

Zaidi ya wabunge 250 wanadaiwa kuunga mkono hoja hiyo ya kumtimua naibu huyo wa rais madarakani.

Comments

Popular posts from this blog

NEMC:Zifahamu fursa zilizopo kwenye taka

APPLICATIONS hizi HAPA haziruhusiwi kutoa mikopo mtandaoni

Geofrey Kiliba, rais mpya wa TAHLISO