Tundu Lissu atangaza kuishtaki Tigo, serikali ya Tanzania

 


Chanzo cha picha,CHADEMALissu

  • Author,

Makamu Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema nchini Tanzania, Tundu Lissu amesema amemuelekeza mwanasheria wake Bob Amsterdam kuanza taratibu za kuishtaki kampuni ya Millicom ambayo ilikuwa kampuni mama ya simu za mkononi ya Tigo kwa pamoja na serikali ya Tanzania kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la kutoa uhai wake.

Lissu ameyasema hayo baada ya mahakama moja nchini Uingereza kuelezwa kuwa kampuni ya mawasiliano ya Tigo (ambayo ilikuwa ikimilikiwa kwa wakati huo na Millicom) ilitoa taarifa za mawasiliano na nyendo za mwanasiasa huyo kwa saa 24 siku chache kabla ya tukio la kushambuliwa kwake.

Septemba 7, 2017 Lissu alishambuliwa kwa risasi zipatazo 16 aliporeja kutoka kwenye kikao cha Bunge, akiwa katika uwanja wa makazi yake na viongozi wengine eneo la Area D, jijini Dodoma, na baadaye kufanyiwa upasuaji mara 25 nchini Kenya na Ubelgiji.

Wakati huo Tundu Lissu alikuwa mbunge wa Singida Mashariki mkoni Singida, katikati mwa Tanzania kupitia Chadema.Hata hivyo, amesema hajui tarehe rasmi ya kuanza kwa kesi hiyo kwani mawakili wake wanahitaji kukusanya ushahidi wa kutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jioni hii, Lissu ameeleza kwanini hakuwahi kufungua kesi dhidi ya Millicom.

"Sikwenda mahakamani kwasababu sikuwa na ushahidi wa kutosha. Lakini sasa tunao ushahidi unaotosheleza kufungua kesi" amesema Lissu.

Comments

Popular posts from this blog

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2025 MAJINA HAYA HAPA.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024.