Posts

Iran inataka kumuua Trump - Idara ya Ujasusi Marekani

Image
  25 Septemba 2024 Idara ya Ujasusi ya Marekani imemuonya mgombea urais kwa tiketi ya Republican, Donald Trump, juu ya kile inachodai ni kitisho cha kweli na cha wazi kutoka Iran inayotaka kumuua. Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump. Brandon/AP Photo/picture alliance MATANGAZO Timu ya kampeni ya mgombea huyo ilisema kwenye taarifa yake ya jana kwamba Ofisi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ilimpa taarifa kwamba kumekuwa na juhudi za wazi za kumuua kutoka Iran, kwa lengo la kuihujumu Marekani na kupandikiza machafuko. Kwa mujibu wa timu hiyo, idara ya ujasusi inaamini kumekuwa matukio ya mashambulizi dhidi ya Trump katika miezi ya karibuni na kwamba imeimarisha ulinzi kwa bilionea huyo anayetaka kurejea madarakani kupitia uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu. Iran inakanusha vikali tuhuma hizo. Marekani inafanya uchaguzi wake mkuu tarehe 5 Novemba, ambapo hadi sasa utafiti wa maoni ya wapigakura yanaonesha kuwa Trump na hasimu wake wa Democrat, Kamala Har...

MAGAZETI YA LEO TAREHE 29-09-2024

Image
                   

Samia asema hajawahi kuua mtu

Image
  Picha:Ikulu Rais Samia Suluhu Hassan. RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema katika maisha yake hajawahi kuua mtu labda sisimizi, huku akiwataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwajibu wale wote ambao wamekuwa wakimshambulia kwa maneno, ikiwamo kumwita muuaji. Alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa serikali katika sherehe za kilele cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Rais Samia alisema amesikia maneno hayo na kwa masikitiko makubwa kwa namna anavyoshambuliwa kuwa yeye ni muuaji ilhali hajawahi kuua mtu. “Sisimizi nimeua lakini mtu sijawahi, sijawahi kuua. Sasa ombi langu kwenu ni kusimama imara. Ukweli  mnaujua mdomo wa Mwenyekiti mmoja kujibu hoja zile hauwezi, pengine mwenyekiti wakati mambo haya yanatokea ninakuwa katika majukumu mengine. “Kwa hiyo msimame muwajibu. Ndugu  zangu, mnahofia nini? Hakuna cha kuhofia hapa. Mkiambiwa  Mwenyekiti na Rais wenu muuaji, waambieni kweli ameua nguvu za upi...

WANYAKYUSA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA MAKUMBUSHO RUNGWE

Image
  Kituo kikubwa cha Makumbusho kabila la Wanyakyusa kujengwa Rungwe Picha:Grace Mwakalinga Patrick Mwalunenge akiangalia vifaa vya asili vya kuvulia samaki vilivyotengenezwa na kabila la Wanyakyusa. JAMII ya Wanyakyusa, wanatarajia kujenga kituo kikubwa cha Makumbusho kitachosheni vitu mbalimbali vitakavyoelezea historia ya kabila hilo, mila, desturi na utamaduni. Akizungumza Septemba 27, 2024 wakati wa kufungua Tamasha la Utamaduni wa Mnyakyusa, linalofanyika kuanzia Septemba 27 hadi 29,  mwaka 2024,  eneo la kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge, amesema kituo hicho kinatarajiwa kujengwa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Mwalunge amesema Tamasha la Jami ya Wanyakyusa linatoa fursa kujadili na kupeana mbinu za namna ya kujikwamua kiuchumi, kushirikiana katika kuenzi na kudumisha mila na desturi. “Tamasha hili litukutanisha watu wa jami ya mbalimbali ya kinyakyusa, tunajifunza namna wazee we...

Lissu asimama kortini kama wakili baada ya miaka saba

Image
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesimama mahakamani kama wakili kutetea kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Singida ikiwa ni miaka saba tangu aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma, Septemba 7, 2017. Wakili Lissu alisimama jana mahakamani kutetea kesi ya jinai inayomkabili Askofu Mwanamapinduzi Machumu Kadutu ambaye amefunguliwa kesi ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya Singida. Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya mahakama baada ya kutoka mahakamani, Wakili Lissu alisema kuwa baada ya kurejea katika kazi ya uwakili kama yangekuwa mapenzi yake, asingependa kusimamia kesi alizodai "za uonevu na hazina kichwa wala miguu" wanazofunguliwa watu. "Kama ingekuwa mapenzi yangu nisiwe ninasimamia hizo kesi, nisiwe ninasimamia watu kwa kesi za uonevu, kama ingekuwa mapenzi yangu watu waache kuonewa, kufunguliwa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu ili mimi nifanye kazi nyingine, kwani muda wangu ni mfupi," alis...

Rais Samia: Sitaki ujauzito shuleni

Image
Rais Samia: Sitaki ujauzito shuleni RAIS Samia Suluhu Hassan ameonya kwamba hataki kusikia kesi za wanafunzi wameshindwa kumaliza masomo yao kutokana na ujauzito na endapo ikitokea atawakaba walimu wao. Alitoa angalizo hilo jana wakati akizindua Shule ya Sekondari Samia Suluhu Hassan iliyojengwa kata ya Rwinga, kijiji cha Migerege, wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma. Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 1,000 wa kidato cha kwanza hadi cha sita. Hadi sasa wanaoendelea na masomo shuleni huko kwa kidato cha kwanza na sita ni 548. "Nisisikie kesi kwamba wanafunzi hawa wameshindwa kumaliza masomo yao kwa sababu ya ujauzito na ikitokea nitakabana shingo na walimu kwa sababu huku msituni hakuna kwa kutokea. "Walimu tunajua kazi tuliyowapeni. Changamoto zenu sisi kama serikali tunazifanyia kazi, tuko pamoja nanyi wala hatutawaacha," aliwaahidi. Rais Samia aliwataka walimu kuhakikisha wanawatunza wanafunzi hao, huku akiwaeleza kwamba Mungu amewachagua kuwa nao. ...

ORODHA YA KWANZA YA WANUFAIKA BODI YA MIKOPO 2024/2025 YATANGAZWA

Image
  Ni awamu ya kwanza yenye wanafunzi 21,509 Mikopo yao ina thamani ya TZS 70.78 bilioni Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumamosi (Septemba 28, 2024) imeanza kutangaza orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo  2024/2025.  Awamu hii ya kwanza inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ya Shahada ya awali, Shule ya Sheria kwa Vitendo na Shahada ya Uzamili. Wanafunzi kupata taarifa kupitia SIPA Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema wanafunzi wote walioomba mikopo kwa mwaka  2024/2025  wanaweza kupata taarifa za kina kuhusu mikopo yao kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama  ‘SIPA’ -  Student’s Individual Permanent Account. “Leo tumeanza kutoa taarifa za mikopo kwa makundi yote, waliopangiwa mikopo, wapo ambao bado tunaendelea kufanyia kazi maombi yao … kila mwombaji anapata taarifa yake kwenye akaunti ile ile aliyotumia kuombea mkopo, huhitaji ku...