Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza nafasi 1,596 za ajira katika kada mbalimbali. Tangazo la nafasi hizo limetolewa leo Alhamisi Februari 6, 2025 na kusainiwa na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo. “TRA inapenda kuajiri watumishi wenye sifa, uwezo na maadili kushika nafasi za kazi katika Idara ya Mapato ya Ndani, Forodha na Ushuru, Usimamizi na Utawala wa Rasilimali Watu, Huduma za Sheria, Menejimenti ya Manunuzi, Utafiti na Mipango, Fedha, Ukaguzi wa Ndani, Mambo ya Ndani na Idara ya Vihatarishi na Uzingatiaji. Kwa hiyo maombi yanaalikwa kutoka kwa Watanzania wenye sifa,”imeeleza taarifa hiyo. Aidha taarifa hiyo imeeleza maombi yote yafanywe kupitia mfumo maalimu wa ajira wa TRA ambao ni: https://recruitment.tra.go.tz/tra careers/User/UserHome.aspx. Kada zilizotangazwa nafasi TRA katika tangazo lake imeeleza nafasi hizo zipo katika kada zifuatazo: Ofisa Msimamizi Ushuru daraja la II (573), Ofisa Forodha daraja la II (232), Msaidizi wa Usimamizi wa Ushuru ...