BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka Watanzania kuanza kubadili mtazamo na kuziona taka kama fursa ya kuzirejeleza na kupata bidhaa mbalimbali na kujikomboa kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa jana, jijini Dar es Salaam na Meneja Utekelezaji wa Sheria wa baraza hilo, Amina Kibola, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amezungumza wakati akizungumzia siku ya kimataifa ya Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Taka, ambayo huadhimishwa kila Machi 30 kila mwaka. Anasema hata kauli mbiu ya mwaka huu, inaweka msisitizo wa kuwa taka si uchafu bali ni malighafi yenye thamani, endapo itasimamiwa na kutumika vyema. Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Amina Kibola, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kibola amesema siku hiyo ilianzishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 2022, ili kukuza mifumo endelevu ya matumizi na uzalishaji na kuongeza uelewa kuhusu udhibiti wa taka. Anasema siku hiyo pia ilianzishwa kwa len...
ENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza application 69 ambazo haziruhusiwi kutoa huduma za mikopo mtandaoni kwa kuwa hazina kibali na haziruhusiwi kuendesha shughuli hizo, huku ikiitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia. Hatua hii inakuja mwezi mmoja tangu Nipashe iibue kero iliyopo kwenye mikopo mtandaoni, huku kasi ya udhalilishaji na utoaji riba kubwa ambao hauna utaratibu wa kisheria hadi BoT ilivyotoa mwongozo kwa watoa huduma hao na kuwataka wajisajili. Licha ya kupewa siku 14, walijitokeza waombaji 16 na kati yake 14 pekee walikidhi vigezo, huku BoT ikichukua hatua kali kwa Microfinance ambazo zilianzisha Apps na kutoa mikopo mtandaoni. Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba: “Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha umma kuwa imebaini kuwepo kwa Majukwaa na Programu Tumizi ‘Applications” zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.” Kupitia taarifa hii, Ben...
Wachezaji watatu wa Singida big stars ambao ni EMMANUEL KWAME KEYEKEH JOSEPHAT ARTHUR BADA MUHAMED DAMARO CAMARA, Ambao waliomba nz wamepewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya sheria ya uraia ya Tanzania , sura ya 357. Kwa muktadha huo kama taarifa ilivyovyotolewa na Idara ya uhamiaji watajwa hapo juu ni Raia wa TANZANIA KWA TAJNISI.
Comments
Post a Comment